Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Ngara mkoani kagera kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo, CHADEMA, Dr Petter Bujari akiwahutubia Wananchi wa Ngara mjini
wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika September 06,2015 kwenye uwanja wa
Posta ya zamani.
Akizungumza
katika mkutano huo wa Kampeni katika Kata ya Ngara mjini,Dr Bujari amesema kuwa
akipewa ridhaa ya Kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara ,atahakikisha anashirikiana na
Wananchi wa Ngara kutumia fursa zinazowazunguka Kuongeza kipato chao, Kusimamia
utawala wa sheria na haki, Kutatua kero na matatizo hasa ya wafanyakazi , walimu
na madaktari aliobainisha kuwa na kero
kubwa ya kunyimwa haki zao pamoja na kuondoa kero za wafugaji na wakulima na
kupanua na kukuza kilimo na ufugaji.
Dr Bujari amesema Wanangara wanapaswa kuwa Wazalendo kwa taifa lao kwa
kufanya maamuzi sahihi kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu 2015 kwa
kuchagua viongozi wenye sifa watakaochochea maendeleo ya Ngara na taifa kwa
ujumla.
|
No comments:
Post a Comment