KAMPENI UKAWA 2015:-Picha zaidi wakati LOWASSA anaingia kwa kishindo katika mkoa wa Singida na kupokelewa na umati wa Wananchi wakiwa na matumaini makubwa ya kupata mabadiliko ya maisha yao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 12, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:-Picha zaidi wakati LOWASSA anaingia kwa kishindo katika mkoa wa Singida na kupokelewa na umati wa Wananchi wakiwa na matumaini makubwa ya kupata mabadiliko ya maisha yao.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.

Mgombea huyo wa Urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh.Edward Lowassa amesema   akichaguliwa kuwa rais hatakuwa na sababu ya kutegemea misaada kutoka nje  kutekeleza ahadi anazotoa na sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA badala yake  atasimamia vizuri rasilimali zilizopo kwani zinatosha kutatua matatizo ya  watanzania.

Baada ya kumaliza kazi ya kufikisha ujumbe wa mabadiliko kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma ambao ni ngome na pia  makao  makuu ya CCM kwa mafanikio makubwa  Mh.Lowasa anaingia kwa kishindo katika mkoa wa Singida na  kupokelewa na   umati wa wananchi wakiwa na matumaini makubwa ya kupata mabadiliko ya maisha yao kupitia ukawa chini ya Mh.Lowasa,ambaye amewaomba kumpa nafasi ya kushughulikia kero  zao kwani anazijua  na  asilimia kubwa ufumbuzi  wake  uko  ndani ya uwezo wake.

Mh.Lowasa ambaye awali amefanya mikutano katika wilaya ya Manyoni,Ikungi na Singida mjini anasema kupitia sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA na uwezo mkubwa wa viongozi na watendaji wana kila  sababu ya kubadilisha maisha ya watanzania kwa muda mfupi  na kwa ufanisi mkubwa...Habari Na:-itv.co.tz/news

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad