Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja
wa CCM mjini Bariadi kwa ajili ya
kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
Wananchi
wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi.
Umati wa
wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano
wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo.
Wananchi
wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa akiwahutubia
mjini Meatu jioni ya leo September 12, 2015.Dkt Magufuli leo ametembelea wilaya
ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,
Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo September 12,2015,mjini Meatu
mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa karibu na
wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu maskini na anajua
nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia ya wakulima na
wafugaji hivyo anajua nini ambacho
anatakiwa kufanya kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo
atahakikisha anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.
Alisema
Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye
wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana
kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba
nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya
maendeleo ya Watanzania wote.
"Nitakuwa
upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda
kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa
kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.
Najua
nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana
wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao
hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.
Aliwataka
wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya
kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali
yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Dk.Magafuli
aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia
nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na
mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye
kazi.
Umati wa
wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye
mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo September 12,
2015.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge na Madiwani kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni
Mwanhunzi,mjini Meatu jioni ya leo mkoani Simiyu.
Wakazi wa
Lamadi ndani ndani ya wilaya ya Busega,Mkoani Simiyu wakishangilia jambo kwenye
mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini humo leo September 12,2015.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Busega,Raphael Chegeni akiwahutubia wananchi wa Busega
mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira
wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
Mwenyekiti
wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM
Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa Busega,mapema leo mchana kwenye mkutano wa
hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza
jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye
mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi
mkoani Simiyu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa
Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.Dkt Magufuli
aliwaomba wananchi hao kuitunza amani waliyonayo na kuwa kuwapuuza wale wote
wenye maneno ya kuleta ufarakanishi katika nchi yetu.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkula,alipokuwa
akipita kuwasalimia wananchi hao akielekea Wilayani Busega kwenye mkutano wa
hadhara.
Maandalizi
ya kumpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ndani ya uwanja wa CCM mjini
Bariadi yalikuwa kama hivyo pichani.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mwanhunzi,alipomaliza
kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mjini
Mwanhunzi,Wilayani Meatu mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment