KAMPENI UKAWA 2015:- Gharika la Lowassa ndani ya Simanjiro, Mkoani Manyara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 26, 2015

KAMPENI UKAWA 2015:- Gharika la Lowassa ndani ya Simanjiro, Mkoani Manyara.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mererani, katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Simanjiro Mkoani Manyara Septemba 25, 2015 ambaye ameahidi kuunda tume maalum itakayojikita kushughulikia matatizo ya wakulima na wafugaji katika eneo la Kiteto mkoani Manyara.

Akiwa mkoani Manyara amehutubia mikutano mikubwa ya hadhara katika maeneo ya Mtui, Kiteto, Merelani na Simanjiro ambapo suala la ardhi lilionekana kumkera na kuahidi kulishughulikia ndani ya miezi miwili tu mara baada ya kula kiapo.
Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara wakionyesha furaha yao mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mererani, Septemba 25, 2015.


Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akivishwa vazi maalum la jamii ya watu wa Kimasai, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara Septemba 25, 2015.
Meneja wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, John Mrema akizungumza na Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akipokea kadi za wanachama wa CCM walioamua kurudisha kadi na kujiunga na UKAWA, wakati wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara Septemba 25, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akizikusanya kadi hizo baada ya kuzipokea.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara.

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ole Zanzibar, Mh. Rajab Mbarouk akiwahutubia  Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad