Celina
Ompeshi Kombani pia alikuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki mkoani
Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amekuwa
mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita. Historia yake Kombani
alizaliwa Juni 19, 1959. Alifariki juzi Septemba 24, 2015 nchini India, ambako
alikuwa anapatiwa matibabu baada ya kugundulika kuwa na saratani. Ameacha mume,
watoto watano na wajukuu wanne.
Alisoma
katika Shule ya Msingi Kwiro wilayani Ulanga mwaka 1968-1975 na Shule ya
Sekondari Kilakala 1975-1978. Baadaye alisoma katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Tabora kwa masomo ya juu ya sekondari mwaka 1979-1981.
Baada ya
masomo ya elimu ya sekondari, Kombani alijiunga na Chuo cha Maendeleo ya
Uongozi Mzumbe (IDM Mzumbe) mwaka 1982-1985 na kati ya 1994-1995 alisomea
Shahada ya Pili ya Uongozi katika Chuo hicho cha Mzumbe.
Kombani
aliwahi kuwa Ofisa Utawala Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)mkoani
Morogoro, Meneja Kiwanda cha Ngozi Morogoro, Ofisa wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kilosa mkoa wa Morogoro, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) mwaka 2008-2010 na Waziri wa Katiba na
Sheria.
Mungu ailaze roho ya Kombani mahala pema peponi.
|
Viongozi
mbalimbali wakiwa katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar
es Salaam tayari kwa kuupokea mwili wa marehemu Celina Kombani. PICHA KWA HISANI YA
KAJUNASON BLOG
|
No comments:
Post a Comment