Mtoto Baraka
Dombeni, akiwa na mama yake Bizimana Violet, akivishwa alama ya utambuzi muda
mfupi baada ya kuwasili jana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, akitokea
Wilaya ya Makamba nchini Burundi. Alama hii ni utambulisho wa kuwawezesha
wakimbizi wanaofika katika kambi ya Nyarugusu kuandikishwa rasmi kabla ya
kupewa hifadhi kambini hapo.
Idadi ya
wakimbizi kutoka Burundi wanaokimbia nchi yao na kuingia nchini Tanzania
imefikia 91,661 kwa takwimu za Jumanne, tarehe 08 Septemba, 2015. Wakimbizi hawa kwa sasa wamehifadhiwa katika
Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.........Kusoma
zaidi bofya HAPA.
|
Afisa
Msajili Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi
(UNHCR), Awadhi Nyanda akichukua taarifa toka kwa familia mojawapo ya wakimbizi
kutoka Burundi wanaoendelea kuingia nchini
kuomba hifadhi. Wakimbizi hawa
wanahifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
Mkoani Kogoma.
|
Mkimbizi kutoka Burundi, Sindaye Salvatory akiwa na
wenzake, akiwekewa alama yake ya utambulisho, wakati walipowasili katika Kambi
ya Wakimbizi ya Nyarugusu jana, wakitokea nchini Burundi kuja kuomba hifadhi
nchini Tanzania kutokana na hali ya kisiasa nchini mwao.
|
Afisa wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, Vivian Vianney akimchukua
alama za vidole mkimbizi kutoka nchini Burundi Bw. Gwasa Jeremia ambaye ni
mmojawapo ya raia wa Burundi wanaoendelea kuingia nchini kuomba hifadhi katika
kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
|
Maofisa wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wanaohusika na
usajili wa wakimbizi wanaopokelewa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarutgusu,
wakiwa katika picha ya pamoja katika Kambi hiyo iliyoko wilayani Kasulu mkoani
Kigoma.
|
Mwakilishi
wa Shirika la OXFAM toka nchini Ireland, Michaelo Riorpan akisaini kitabu cha
wageni alipowasili na wenzake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu jana. Shirika la OXFAM linatoa misaada mbalimbali
kusaidia utoaji wa huduma za maji na utunzaji wa mazingira katika Kambi ya
Wakimbizi ya Nyarugusu. Aliyesimama ni
Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B) Bw. Fredrick Nisajile ambaye aliupokea ugeni
huo.
|
Mkimbizi
kutoka Burundi akipata huduma ya maji katika moja ya vituo vya maji
vilivyojengwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Huduma za maji safi na salama ni mojawapo ya
mambo yanayotiliwa mkazo ili kulinda afya za wakimbizi.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
|
No comments:
Post a Comment