WIKI HII MASIKIO YOTE DODOMA:- Nani atakaye mrithi Kikwete katika CCM? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 08, 2015

WIKI HII MASIKIO YOTE DODOMA:- Nani atakaye mrithi Kikwete katika CCM?


Wiki hii maskio yote ya Watanzania yanaelekezwa mjini Dodoma, mji mkuu wa Tanzania ambapo chama tawala nchini humo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinamchagua mtu mmoja atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba 2015.

Vikao vya mchakato huo vinaanza rasmi Jumatano huku vikitanguliwa na kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo kimsingi pamoja na mambo mengine kitapitia wasifu wa watia nia wote lakini pasipo kupunguza jina lolote.

Siku ya Alhamisi (09 Julai), Kamati Kuu ya chama yenye wanachama takribani 32 itakutana na hapo ndipo upungazaji wa majina utafanyika hadi kufikia majina matano tu.

Rais Kikwete ndiye anayeondoka.

Baada ya hapo, Halmashauri kuu ya chama itakutana siku ya Ijumaa tarehe 10 Julai,2015  ambapo itachuja majina hayo matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga kura. Majina haya matatu ndiyo yatakayokwenda katika Mkutano Mkuu wa Chama ambao ndio utakaochagua jina moja la huyo mgombea urais kwa tiketi ya chama.


Leo ,Julai 08,2015 kikao cha usalama na maadili, kinakaa chini ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Kesho asubuhi kutakuwa na ufunguzi wa ukumbi mpya wa CCM na ofisi zake, kabla ya Rais Kikwete kwenda bungeni mchana kwa ajili ya shughuli za kuvunja Bunge.

Aidha, mchana kutakuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM. Keshokutwa NEC itateua jina la mgombea urais wa Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Nape, kazi nyingine itakayofanyika siku hiyo ya Julai 10 ni kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Uchaguzi 2015 - 2020 , ambayo itatumika kuombea kura. Ilani hiyo itapelekwa kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuhitimishwa.

Mkutano Mkuu huu unajumisha takribani wanachama 2100 ikiwa ni pamoja na Wabunge wa CCM Tanzania bara na wawakilishi wengine kutoka Zanzibar lakini pia wawakilishi wa chama kutoka ngazi mbalimbali hadi zile za chini.

Mkutano huu umepangwa kufanyika tarehe 11 hadi 12 Julai,2015,ambapo
Kwa mara ya kwanza katika historia ya CCM na nchi kwa ujumla, idadi ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu na kusaka ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho ilifikia 42.


Mwaka 1995 kulikuwa na wagombea 17, mwaka 2005 wagombea walikuwa 11 na mwaka huu waliorudisha fomu na kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha urais ni wagombea 38.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad