Jaji Mstaafu, Joseph Warioba.
RAIS Jakaya Kikwete ametakiwa
kujivua mapenzi yake kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kutenda haki katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … Mwanahalisi Online.
Mbali na Kikwete kutakiwa kujivua
mapenzi kwa chama chake pia, CCM imetakiwa kutopitisha watangaza nia wenye doa
(kashfa mbalimbali) ili kulinda maslahi mapana ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo Julai
08,2015, jijini Dar es Salaam na jopo la watoa mada katika kongamano la
kujadili “Amani na umoja kuelekea uchaguzi mkuu” lililoandaliwa na Taasisi ya
Mwalimu Nyerere.
Akizungumza katika kongamano hilo
Humphrey Polepole, aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema
kama CCM itapitisha wagombea urais wenye doa, wakaachwa kufanya michezo kama
walivyofanya michezo katika suala la katiba.
Atahadharisha wananchi kutopigia
kura CCM.
“Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kusema
CCM ikataliwe. Nitasema bila hofu…Watanzania eeeeh… naomba muwanyime CCM Kura
zenu. Haya mambo ya kufanya michezo na maendeleo sipo tayari kuyaona.
Mbali na kuikemea CCM, Polepole
ameutaka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuacha ubinafsi kwa kuwa kufanya
hivyo ni kubomoa misingi ya demokrasia.
Katika kongamnao hilo, Jaji Kiongozi
Mstaafu Amir Ramadhan Maneto amesema, “Haki ndio inazaa amani.”....“Tunataka haki itendeke bila ubaguzi
wowote. Ndipo amani itakuwepo. Hivyo kuelekea uchaguzi mkuu, Rais Kikwete
ajitoe kwenye chama chake. Haki itatendeka,” amesema Maneto ambaye aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.
Amesema viashiria vinaonesha
serikali ndio chanzo cha kuvunjika kwa mani hasa katika kipindi cha uchaguzi.
Maneto amelishutumu Jeshi la Polisi,
kitengo cha Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kutumika kuanzisha fujo katika
maeneo kadhaa ikiwemo mauaji ya David Mwangosi, aliyekuwa mwandishi wa habari
wa kituo cha televisheni cha Channel Ten katika kijiji cha Nyololo mkoano
Iringa mwaka 2012.
Profesa Mwesiga Baregu, ambaye
alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema,”…kama uchaguzi
hautoonekana kuendeshwa kwa haki. Na matokeo yake sio ya haki, tutakuwa
tunavunja amani.”
“Tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa na
obwe la Katiba. Tulikubaliana kabla ya uchaguzi mkuu ni lazima tuwe na: tume
huru ya uchaguzi; mgombea huru; uwezo wa kuhoji matokeo ya rais na rais
achaguliwe kwa kura zaidi ya asilimia 50. Yote hayo hatuna. Viashiria vyote
vinafanana na yaliyotokea Kenya mwaka 2007 na 2008,” amesema Baregu.
Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu
Mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema,
“…waasisi wa taifa hili walitanguliza utu, haki na usawa. Walisimamia misingi
hiyo. Wagombea 38 ni wengi. Kila mmoja ametoa ahadi.
Hawatumii Ilani ya chama.
Wengine tunajiuliza ni wagombea binafsi?.”
“Wale ambao wataenda kuwapima
wagombea tayari wamejitokeza kuwaunga baadhi ya wagombea. Wao ndio wanaenda
kuamua. Je watatenda haki?,” amehoji Warioba.
Pia, Awadhi Ali Said, aliyekuwa
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ameeleza kuwa kila mara uchaguzi mkuu
katika nchi za Afrika huacha makovu ya machafuko au kutokuwepo kwa maridhiano.
“Ni muhimu kuhoji, muungano wetu wa
miaka 50 una amani?, una umoja?, una utulivu?. Unapogusia afya yake ni kama
unaunyanyapaa kama vile ni jambo ambalo hatutakiwi tulifanye,” amesema Said.
|
Wednesday, July 08, 2015
AMANI NA UMOJA KUELEKEA UCHAGUZI 2015:- Warioba, Polepole, Baregu waipopoa CCM.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment