UBUNGE JIMBO LA NGARA 2015:- Bw Cyprian Muheranyi Atangaza nia kupitia CCM huku akiahidi kusimamia Utawara bora na Uwajibikaji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 08, 2015

UBUNGE JIMBO LA NGARA 2015:- Bw Cyprian Muheranyi Atangaza nia kupitia CCM huku akiahidi kusimamia Utawara bora na Uwajibikaji.

Imeelezwa kuwa wakazi wa wilaya ya Ngara wanakabiliwa na Changamoto mbalimbali zinazohitaji Mwakilishi sahihi kuzishughulikia ili kuchochea Maendeleo ya Ngara na Mkoa wa Kagera kwa Ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uchumi Mmwandamizi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw Cyprian Muheranyi ambaye ni Mzaliwa wa Bukiriro wilayani Ngara muda mfupi baada ya kutangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Ngara,Mkoani Kagera kupitia Chama cha Mapinduzi,CCM.

Bw Muheranyi anayewania nafasi hiyo kwa mara ya 3 sasa ,amesema kiongozi bora ni yule asiyekata tamaa hata pale kura zake zinaposhindwa kutosha na kwamba iwapo atachaguliwa atashughulikia upatikanaji wa Huduma bora ya maji mjini na Vijijini pamoja na kushughulikia huduma za Matibabu kwenye zahanati na Vituo vya Afya.

Bw Muheranyi amesema Iwapo atateuliwa na CCM na kisha kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu,2015 atahakikisha anasimamia Haki za Makundi yote ya Kijamii wakiwemo Walemavu, Yatima, Watoto, Wajane na Wazee aliodai kuwa wamesahaulika.

Bw Muheranyi anaungana na watia nia wengine ambao ni Dr.Philimon Sengati,Alex Gashaza na Mwl.Jerad Muhile kupitia CCM huku CHADEMA akitangaza nia Dr.Petter Bujari kuomba kuteuliwa na Vyama vyao ili kuwania Ubunge wa Jimbo la Ngara.

Source:-Radio Kwizera FM.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad