MAKUBALIANO YETU:-Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 08, 2015

MAKUBALIANO YETU:-Mayweather apokonywa taji alilomshinda Pacquiao.

Mayweather (Pichani ) apokonywa taji alilomshinda Pacquiao.

Bondia Bingwa wa dunia wa uzani wa Welter, Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Mei,mwaka huu.

 Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 38 anadaiwa kushindwa kuilipa shirikisho la ndondi la WBO ada ya dola laki mbili, $200,000 kabla ya makubaliano aliyopewa ya tarehe 3 Julai,2015.

Mayweather alitakiwa pia kutoa ukanda wa chipukizi wa WBO punde baada ya kumshinda mfilipino Pacquiao kwa wingi wa alama.

Kufuatia kauli hiyo ya shirikisho la ndondi la WBO, Mayweather hatambuliwi tena kama mshikilizi wa taji hilo.


Taswira Floyd Mayweather amepokonywa ukanda alioutwaa baada ya kumchapa Mfilipino Manny Pacquiao mwezi Me,2015 Pichani kulia,sasa Taji hilo linashikiliwa na Mmarekani mwenza Timothy Bradley.

Yamkini Mayweather alikuwa ameiahidi WBO kuwa akimshinda Pacquiao,angevua mataji yote ya vijana ilikuwapa mabondia wapya fursa ya kuwania mataji hayo lakini hadi kufikia sasa hajafanya hivyo.

Taarifa yao iliyochapishwa katika mtandao wa www.boboxing.com imesema kuwa ''hatukukuwa na lingine baada ya Mayweather kushindwa kutekeleza matakwa yetu.kwa hivyo hatutamtambua mayweather kama mshikilizi wa ukanda huo wa Welter''.
Mayweather, ambaye ndiye anayeshikilia mataji ya WBA na WBC ana hadi julai tarehe 20,2015 kukata rufaa ya kauli hiyo. 

Mayweather anatarajiwa kuandaa pigano lingine mjini Las Vegas tarehe 12 Septemba,2015 japo haijabainika atazichapa dhidi ya nani.

Wakati hayo yakijiri WBO inapanga pigano la welter linalopangwa kufanyika tarehe 27 kati ya Bradley na Jessie Vargas.

Source:-BBS Swahili.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad