Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, akisoma hotuba ya
kuhimisha mkutano wa 20 wa Bunge mjini Dodoma jana Julai 09,2015. Picha na Emmanuel Herman .
Rais Jakaya
Kikwete anamaliza utawala wake kwa kuongeza maeneo mapya ya utawala, baada ya
kuridhia kuanzishwa kwa wilaya mpya sita na mkoa mmoja wa Songwe utakaofanya
nchi kuwa na mikoa 31.
Akitoa
hotuba ya kuahirisha Bunge hadi itakapotangazwa kwenye Tangazo la Serikali,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kuwa Rais Kikwete ameridhia uanzishwaji wa
mkoa huo uliomegwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Alisema pia
zimeongezwa wilaya mpya sita, zikiwamo Ubungo na Kigamboni za mkoani Dar es
Salaam, halmashauri 25 za wilaya, halmashauri 17 za manispaa na miji, tarafa
tano na kata 586.
Pinda
alisema Serikali imeamua kuanzisha maeneo hayo ya utawala ili kusogeza utawala
kwa watu na kuchagiza maendeleo nchini kwa kurahisisha utoaji wa huduma kwa
wananchi.
“Halmashauri
za wilaya zilizoanzishwa ni Buchosa, Malinyi, Madaba, Manyoni, Mpimbwe, Nsimbo, Buhigwe, Nyang’wale, Kankonko Uvinza, Mlele, Mbogwe, Buhigwe,
Momba, Butiama, Ushetu, Nyasa, Busega, Msalala, Ikungi, Mkalama, Itilima,
Ikungi, Bubumburi na Kariua,” alisema Pinda.
Pamoja na
halmashauri hizo za wilaya, kiongozi huyo mkuu wa shughuli za Serikali alisema,
Serikali imeongeza manispaa na miji mipya ambayo ni Chalinze, Ifakara,
Nanyamba, Newala, Kondoa, Mafinga, Mbulu, Bunda, Mbinga, Tunduma, Nzega,
Handeni, Kasulu, Geita, Masasi, Manispaa ya Ilemela na Kahama.
“Pia,
mheshimiwa rais ameridhia kuanzishwa tarafa tano ikiwemo ya Mchemwa iliyopo
Newala na tarafa nne za Tandahimba ambazo ni Mchichila, Mihambwe, Mambamba,
Namangombya.
“Aidha,
tumeanzisha kata mpya 586… mheshimiwa spika inawezekana orodha haijatoa taarifa
za kina, lakini tunaweza kuisahihisha tutakapokuwa tunatoa kwenye tangazo rasmi
za Serikali siku zijazo,” alisema Pinda.
Katika
hotuba hiyo, Pinda alisema kazi ya kuanzisha maeneo mapya hufanywa kila baada
ya muda fulani kutokana na mazingira, ongezeko la watu pamoja na vigezo
mbalimbali na anaamini litazidi kuimarisha utendaji na shughuli za maendeleo
nchini.
Pinda pia
alitumia hotuba hiyo kueleza mafanikio mbalimbali ya Serikali ya awamu ya nne
katika sekta zote huku akisisitiza kuwa wataongeza jitihada za kuziba mianya ya
ukwepaji kodi ili kuongeza mapato nchini.
Kuhusu
uandikishaji wapiga kura, Pinda alisema
hadi sasa kazi hiyo imekamilika katika halmashauri za mikoa 13 ya Njombe,
Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Dodoma, Katavi, Rukwa, Singida, Tabora,
Kagera, na Kigoma.
Alisema Tume
ya taifa ya Uchaguzi (NEC) imevuka lengo kwa kuandikisha watu 11,248,194 wenye
sifa za kupiga kura na malengo ya Tume ni kuandikisha kati ya watu milioni 21
hadi 23.
Source:-Gazeti
la Mwananchi Julai 10,2015.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, July 10, 2015
KUSOGEZA HUDUMA:-Huu ndio Mkoa na wilaya sita mpya, zilizotangazwa na Serikali.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment