MAFANIKIO:- Taswira Picha Okwi akitambulishwa na Klabu ya SONDERJYSKE ya Denmark baada ya Usajili kukamilika. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 10, 2015

MAFANIKIO:- Taswira Picha Okwi akitambulishwa na Klabu ya SONDERJYSKE ya Denmark baada ya Usajili kukamilika.

Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Simba SC, Emmanuel Okwi ametambulishwa katika klabu ya Sonderjyske inayoshiriki katika ligi kuu ya Denmark. 

KLABU ya SonderjyskE FC ya Ligi Kuu ya Denmark imesaini Mkataba wa miaka mitano na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ahamishie huduma zake klabu ya Haderslev kutoka Simba SC ya Tanzania.

Okwi mwenye umri wa miaka 22, sasa atakuwa analipwa dola za Kimarekani 10,000 kwa mwezi, akipatiwa nyumba, usafiri na huduma nyingine zote muhimu Denmark.

Tovuti ya klabu hiyo imesema makubaliano baina ya Okwi na klabu yake ya zamani, Simba SC yamekamilika na sasa taratibu za usajili zinaendelea baada ya jana Julai 09,2015 kukabidhiwa jezi namba 25 aliyokuwa anatumia Tanzania.

Kocha Hans Jorgen Haysen amesema kwamba Okwi ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa, kasi, nguvu na utaalamu wa hali ya juu.
Okwi akikabidhiwa jezi namba 25 jana baada ya kusaini Mkataba wa miaka mitano na Sonderjyske FC.

Ana jina kubwa sana Tanzania na Uganda, ambako ameonyesha umahiri wake mkubwa wa kufunga katika klabu na timu ya taifa,”amesema.

Okwi aliyeifungia mabao 18 timu ya taifa ya Uganda katika mechi 35, msimu uliopita aliichezea Simba SC akitokea kwa mahasimu, Yanga SC ambako pia alicheza kwa nusu mwaka kabla ya kutofautiana na viongozi wa klabu hiyo na kuondoka.

Simba SC ndiyo iliyomuingiza Tanzania Okwi mwaka 2010 akitokea SC Villa ya kwao. Alicheza Msimbazi hadi mwaka 2013 aliponunuliwa na Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola za KImarekani 300,000 (Sh. Milioni 600 na zaidi).

Hata hivyo, Okwi aliondoka Tunisia baada ya miezi mitatu kufuatia kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo na baadaye kufungua kesi FIFA akiomba aruhusiwe kucheza klabu nyingine kulinda kipaji chake wakati mgogoro wake na Etoile unaendelea.

Etoile ilisitisha huduma kwa Okwi, baada ya kukerwa na desturi ya mchezaji huyo kuchelewa kurejea kujiunga na timu anaporuhusiwa kwenda kujiunga na timu yake ya taifa Uganda.

Akasaini tena SC Villa katikati ya mwaka 2013 kabla ya Desemba mwaka huo, kuhamia Yanga SC- wakati wote huo kesi yake na Etoile ikiendelea FIFA. 

Hata hivyo, Agosti mwaka jana, Okwi akarejea Simba SC kwa Mkataba wa miaka miwili kabla ya mwezi huu kuhamia Denmark. 

Etoile haikuwahi kuilipa Simba SC fedha za manunuzi ya Okwi na klabu ya Tanzania ilifungua kesi FIFA ikashinda, timu ya Tunisia ikiamriwa hadi katikati ya mwaka jana, lakini hadi leo haijafanya hivyo.

Lakini sasa Simba SC inaweza kupoza machungu iwapo SonderjyskE FC itatoa dau zuri, ambalo hadi sasa ni siri yao.

Source:-BIN ZUBER

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad