Rais Jakaya
Kikwete akihutubia wakati akilivunja Bunge mjini Dodoma jana Julai 09,2015.
Kulia ni Spika wa Bunge Anne Makinda. Picha na Edwin Mjwahuzi.
Rais Jakaya
Kikwete amelihutubia Bunge la 10 kwa mara ya mwisho, akijikita katika takwimu
zinazoonyesha mafanikio ambayo Serikali ya Awamu ya Nne imeyapata tangu
alipoingia Ikulu mwaka 2005, lakini akakiri kutofanikiwa kulifufua Shirika la
Ndege Tanzania (ATCL).
Hali
iliyokuwa mwaka 2010 wakati alipohutubia Bunge hilo kwa mara ya kwanza, ndiyo
iliyojirudia jana Julai 09,2015, baada ya wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao na kuwaacha wapinzani wachache.
Rais
Kikwete, ambaye alihutubia kwa saa 2.20 alitangaza kulivunja Bunge la 10 lakini
akasema litavunjwa rasmi Agosti 20,2015, akieleza kuwa shughuli ya jana ilikuwa kama
“kitchen party au send off”.
Katika
hotuba yake, Rais Kikwete alimmwagia sifa Spika Anne Makinda, wabunge wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali, wananchi
na chama chake kwa kumuamini, huku akisisitiza kuwa anaondoka madarakani na
kuiacha nchi ikiwa salama.BOFYA HAPA KUSOMA - Hotuba ya Rais Kikwete Wakati wa Kuagana na Wabunge na Kulivunja Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
|
Friday, July 10, 2015
KATIBA YETU:-JK avunja Bunge, ataja mafanikio ya miaka 10.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment