Wabunge wa
Upinzani wakitoka nje ya Bunge.
SPIKA wa Bunge, Anne
Makinda, amewafukuza bungeni wabunge wengine 35 wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni baada ya kuwafukuza wengine 11 jana. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
'' Kutokana na hali
hiyo, wabunge wa upinzani waliofukuzwa kati ya juzi na jana wamefikia 46 kati
ya wabunge 90 wa kambi hiyo.
Tukio la wabunge 35
kufukuzwa, lilitokea bungeni jana saa tatu asubuhi muda mfupi baada ya Spika
huyo kusoma dua ya kuliombea Bunge.
Baadhi ya
waliofukuzwa jana kwa upande wa Chadema ni pamoja na Ezekia Wenje (Nyamagana),
Mustafa Akunay (Mbulu), Israel Natse (Karatu), Lucy Owenya (Viti Maalum), Grace
Kiwelu (Viti Maalum) pamoja na Profesa Kulikoyela Kahigi (Bukombe).
Kwa upande wa Chama
cha Wananchi (CUF), waliofukuzwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Mashirika ya Umma, Amina Mwidau (Viti Maalum), Salum Baruani (Lindi
Mjini), Musa Haji Kombo (Chakechake) na Mbunge wa Mgogoni, Kombo Hamis Kombo.
Pamoja na kuwafukuza
bungeni, Spika Makinda alisema wabunge hao hawataruhusiwa kuhudhuria vikao
vitano vya Bunge vilivyobaki kabla Bunge halijavunjwa wiki ijayo.
Kabla wabunge hao
hawajafukuzwa jana, Wenje alisimama na kuomba mwongozo wa Spika zikiwa ni
dakika chache kabla Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawe,
hajawasilisha kwa hati ya dharura miswada mitatu inayopingwa na wabunge hao.
Miswada hiyo ni
Muswada wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa
Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Uwazi na
Uwajibikaji Katika Tasnia ya Uchimbaji Tanzania wa Mwaka 2015.
Katika mwongozo wake,
Wenje alihoji ni kwa nini askari wa Bunge walimzuia kuingia bungeni jana,
Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) wakati jina lake haliko
kwenye orodha ya wabunge waliozuiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kuanzia juzi.
Aidha, alitaka kujua
ni kwanini Serikali inataka kuwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu
masuala ya petroli, gesi na mafuta kwa hati ya dharura wakati miswada hiyo
imekataliwa na wabunge pamoja na wadau wa sekta ya nishati nchini.
Akijibu mwongozo huo,
Spika Makinda alisema Mbunge Silinde ni kati ya wabunge waliofungiwa kuhudhuria
vikao vya Bunge kuanzia juzi kwa kuwa alishiriki kufanya fujo juzi.
“Silinde hatakiwi
kuhudhuria na kama hakutajwa katika orodha jana (juzi), jina lake lilisahaurika
tu kwa sababu naye nilikuwa nimemtaja.
“Kuhusu miswada
mitatu kuwasilishwa kwa siku moja, hakuna kanuni iliyokiukwa na wanaolalamikia
hilo, hawajui kanuni zinasemaje ingawa wamekaa bungeni kwa muda mrefu,” amesema
Spika Makinda.
Baada ya kusema
hivyo, Wenje alisimama na kuanza kumlalamikia Spika akisema anawaonea wabunge
wa upinzani kwa kuwa anaipendelea Serikali.
“Mheshimiwa Spika
unatuonea, Silinde hakutajwa katika orodha ya waliozuiwa kuingia bungeni na
kama jina lake lilirukwa kama unavyosema, wewe huna mamlaka ya kumzuia kuingia
hapa kwa mujibu wa kanuni za Bunge hadi upate mapendekezo ya Kamati ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge,” alilalamika Wenje.
Kauli hiyo ilionekana
kumkera Spika kwani alisimama na kutishia kumfukuza bungeni Wenje kwa kile
alichosema anavunja kanuni za Bunge na mvutano kati yao ulikuwa hivi.
Spika: Wenje naona unatumia delaying
tactics, kama hutaki kutulia utaondoka hapa kwa sababu nimeshakwambia jina la
Silinde lilirukwa tu lakini hatakiwi kuwa hapa.
Wenje: Usitake kutumia vitisho, mimi
siwezi kuogopa kufukuzwa kwa sababu haitakuwa mara ya kwanza kufukuzwa hapa.
Spika: Wenje unaongea bila kufuata
utaratibu itabidi sasa utolewe nje.
Wenje: Mheshimiwa Spika, nakwambia
unatuonea, sijawahi kuona Bunge lolote duniani likiwasilisha miswada mitatu kwa
wakati mmoja, wewe tuonee tu.
Spika: Sasa nasema Wenje atolewe nje na
hatahudhuria vikao vitano kuanzia sasa.
Spika alipotoa uamuzi
huo, Wenje alitoka nje akiongozwa na askari wa Bunge huku wabunge wote wa Kambi
ya Upinzani wakiwa wamesimama na kuanza kupiga kelele wakitaka wafukuzwe wote.
Kauli hiyo
ilimsimamisha tena Spika na kuwaambia wabunge hao. Kama mnataka kufukuzwa
endeleeni kusimama ili niwaandike majina baadaye niwafukuze.
Spika aliposema
hivyo, wabunge hao walisema kwa pamoja, tutasimama, tuandike vizuri.
Baada ya hapo,
maofisa wa Bunge walianza kuandika majina hayo na kisha walimkabidhi orodha
hiyo Spika Makinda ambaye aliisoma na kuwafukuza bungeni akitumia kanuni ya
Bunge ya 74 (1).
Kutokana na uamuzi
huo, miswada hiyo iliwasilishwa kwa mujibu wa ratiba ya Bunge kisha wabunge
waliichangia.
Sakata la wabunge
kupiga miswada hiyo, lilianza Juni 29 mwaka huu 2015 wakati wabunge wote
walipokutana na wadau wa sekta ya nishati kujadili miswada hiyo mjini Dodoma.
Wakati wa semina
hiyo, wabunge wa upinzani na CCM waliungana kuipinga miswada hiyo ambapo Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage, alimrushia maneno ya kashfa
Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM) baada ya mbunge huyo kuikataa miswada
hiyo.
Source:- MWANAHALISI..
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Saturday, July 04, 2015
BUNGENI DODOMA:-Makinda azidi kuwafagia UKAWA, atimua wengine 35.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment