Akizungumza
katika kongamano hilo la wazee la kutafakari uchaguzi wa mwaka 2015, Dk Slaa
alisema ingawa wazee waliungana na Hayati Mwalimu Nyerere kupambana na maadui
wa tatu ambao ni ujinga, umaskini na maradhi lakini kwa sasa ameongezeka adui
wa nne ambaye ni ufisadi.
“Ujinga
alioupinga Mwalimu na wazee umeondoka? Lakini ujinga, umaskini na maradhi na
kuna adui wa nne ambaye ni ufisadi,” alisema.
Alisema
hakuna Mtanzania ambaye atakwenda dukani na Sh10,000 kununua chumvi na kibiriti
halafu akaacha chenji yake dukani kwa makusudi na hivyo Watanzania bado wanadai
fedha zao zilizopotea kutokana na ufisadi.
Kadhalika Dk
Slaa alisema kitendo cha wazee hao kukutana katika kongamano hilo kinaashiria
kuwa wana kiu, njaa na matumaini ya kutaka mabadiliko.
“Mwalimu pia
alipokewa na wazee wa Bagamoyo ambao walimuombea dua, akaenda kwenye makaburi
na waliunganisha nguvu kumng’oa Mwingereza na kupata uhuru na mimi nawataka
wazee wa Dar es Salaam kuongeza nguvu kuing’oa CCM,” alisema Dk Slaa.
Alizungumzia
pia uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura na kuwataka wakazi wa Dar
es Salaam kuwa makini na kuhakikisha wanajiandikisha.
Awali,
katika kongamano hilo, Naibu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na Shura
za Maimamu nchini Sheikh Rajab Katimba aliizungumzia kauli ya Katibu wa Itikadi
na Uenezi, wa CCM Nape Nnauye ya kuwa CCM itashinda kwenye Uchaguzi Mkuu ujao
hata kwa bao la mkono na kusema ni ya kichochezi.
“Wakati nchi
inajitahidi kuwa na amani na kuwa na uchaguzi wa haki na huru, kiongozi wa
chama anazungumza uchochezi mkubwa ambao kama viongozi wengine wangeusema
sidhani kama wangekuwa salama,” alisema.
Sheikh
Katimba aliwaasa Ukawa kuwa na umoja na kuwataka wawaite wazee ili wawape
ushauri badala ya kulumbana kwani huu si wakati mwafaka wa kuwa na migogoro.
No comments:
Post a Comment