UBUNGE JIMBO LA NGARA 2015:- Alex Gashanza aomba ridhaa ya CCM na Ndoto ya kuhakikisha miundombinu ya uchumi inaimarika hasa kuwa na viwanda vya mazao ya wakulima na wafugaji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 04, 2015

UBUNGE JIMBO LA NGARA 2015:- Alex Gashanza aomba ridhaa ya CCM na Ndoto ya kuhakikisha miundombinu ya uchumi inaimarika hasa kuwa na viwanda vya mazao ya wakulima na wafugaji.

Alex Gashaza ( Pichani ) ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima, (TCCIA) wilayani Ngara ambaye jana Jully 03,2015 ametangaza kuwania Jimbo la Ngara  kumrithi Mbunge wa sasa  Deogratias Aloyse Ntukamazina kupitia CCM.

 Anasema kuwa kiongozi  na mtawala bora kidemokrasia  ni yule anayejitoa kutumikia wananchi wala si kutumika kwa maslahi yake, ambapo anahitaji kuitwa mtumwa wa watawaliwa ili kutatua kero za watu anaowaongoza.

Miongoni mwa ndoto zake za uongozi  katika kukabiliana na changamoto zilizopo kwa wananchi, kuhakikisha miundombinu ya uchumi inaimarika hasa kuwa na viwanda vya mazao ya wakulima na wafugaji.

Anadai wilaya ya Ngara ni kubwa yenye ardhi iliyo na rutuba ya kutosha ambayo imejaa mabonde kwa ajili ya kilimo takriban Hekta 5000, ambapo wananchi wakipata wataalamu wa kilimo na mifugo  wanaweza kujiinua kiuchumi

Amesema  akichaguliwa kuongoza jimbo hilo, ataanzisha uzalishaji wa zao la Stevia ambalo linatumika kutibu ugonjwa wa kisukari ambalo kwa sasa  linafanyiwa utafiti duniani kutumika badala ya kilimo cha zao la miwa.

Amesema zao  la Stevia limastahimili kwenye mabonde ambayo yamejaa wilayani humo ambapo kilo moja ya zao hilo huuzwa kwa dola 2 za Kimarekani na katika ekari moja huzalishwa kiasi cha tani mbili kila baada ya miezi mitatu.

Mchuano wa mwaka 2010 ulikuwa mkali uliohusisha wagombea 10 kutoka CCM na yeye kuwa mshindi wa pili katika kura za maoni,alipata kura 4,922 huku mbunge wa sasa Deogratias Ntukamazina akipata kura 5,563

Kutokana na mchuano huo aliteuliwa na CCM wilayani Ngara kuwa Kampeni Meneja wa Ntukamazina, akiambatana na wapambe wengine kumuombea kura  kwa wananchi ambapo mgombea huyo alipelekwa India kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua.



Hata hivyo amesema ili kukuza uchumi wa wakazi wa Ngara endapo wananchi wakishirikiana na wataalamu watakaokuja kuwekeza zao hilo  watajipanua  na kukuza uchumi wao kwa lengo la kupunguza umaskini kwenye wilaya hiyo.
 
 Alianza  kufahamika baada ya kuhitimu masomo yake ya uhandisi na usanifu wa majengo katika chuo cha Ufundi cha Mbeya ( Mbeya Technical) na  katika kuwania jimbo hilo harakati zake zilianza mwaka 2000 akiwa mwananchama wa NCCR  Mageuzi.

Wakati huo alichuana na mbunge wa zamani Angasi Gwassa Sebabili ambapo ndoto za ubunge hazikutimia  kisha kutupa karata yake  mwaka 2005 baada ya  kurejea CCM akichuana na  Profesa Feedham Banyikwa na kukosa nafasi hiyo kwa mara ya pili.






Alex Raphael Gashaza ni mkazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera aliyezaliwa katika kijiji cha Murukulazo Agost 30 , 1967 ambaye alisoma shule ya msingi ya kijiji hicho kwa kuhitimu  elimu ya msingi  mwaka 1983 akiwa wilayani Ngara.

Alipohitimu elimu ya Msingi alichaguliwa  kujiunga na shule maalum ya kilimo  ya kilosa mkoani Morogoro akiwa miongoni mwa wanafunzi 20 wa mkoa wa kagera waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo mwaka 1984 hadi mwaka 1987.

Baadaye alijiendeleza katika chuo cha Ufundi Mbeya na kuhitimu kidato cha sita katika masomo ya PCM kisha kujiunga na JKT Makutupora  mkoani Dodoma ambapo alianza kujiajiri wilayani Ngara akiwa Msanifu wa makazi ya wakimbizi wilayani humo mwaka 1993.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad