RIDHAA UBUNGE JIMBO LA NGARA:-Bw.Jared Muhile atangaza nia kupitia CCM na robo ya mshahara wake atautumia kwa shughuli za maendeleo kila kata ikiwa Atachaguliwa . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 22, 2015

RIDHAA UBUNGE JIMBO LA NGARA:-Bw.Jared Muhile atangaza nia kupitia CCM na robo ya mshahara wake atautumia kwa shughuli za maendeleo kila kata ikiwa Atachaguliwa .

Aliyewahi kuwa  Mkuu wa shule ya Sekondari LUKOLE kabla ya kuteuliwa Afsa Elimu Taaluma wa wilaya Ngara mkoani Kagera Bw.Jared Muhile akipokelewa na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mumiterama leo June 22, 2015 wakati akiwasili kwenye  viwanja vya shule ya msingi Mumiterama na kutangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ngara kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

 Pamoja na mambo mengine amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya Chama chake katika kuwania Ubunge wa Jimbo la Ngara  kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Bw.Jared Muhile  amewataka wana Ngara ,’’-wampime kwa mambo aliyokwisha Fanya wakati akiwa Mkuu wa shule Mugoma na LUKOLE sambamba na  usimamiz wake uliotukuka akitolea mafanikio aliyoyaleta katika sekta ya Elimu kwa kuitoa wilaya ya NGARA nafasi ya Mia na........ Mpaka nafasi ya therathin na....hivyo kiusimamizi yupo vizuri.
Umati wa wanaCCM na Wananchi wa Mumiterama , ukimsikiliza  kwa furaha, Aliyewahi kuwa  Mkuu wa shule ya Sekondari LUKOLE kabla ya kuteuliwa Afsa Elimu Taaluma wa wilaya Ngara mkoani Kagera Bw.Jared Muhile (hayupo pichani) wakati alipopanda jukwaani kuwahutubia leo June 22, 2015 wakati anatangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Ngara kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.






Bw.Jared Muhile (pichani) akiwahutubia wana CCM na Wananchi wa Mumiterama ,wilayani Ngara mkoani Kagrea na kuwataka  wanangara katika uchaguzi wa safari hii kuwa makini na wachagua Mbunge  msomi mzawa na mkazi wa Ngara na kwamba kama chama kitampa nafasi na kuchaguliwa na Wana Ngara kuwa Mbunge wao ,atatumia robo ya mshahara wake kwa shughuli za maendeleo kila kata na kwa muda wote wa ubunge wake.



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad