SIMBA SPORTS CLUB:-Ifahamu Tovuti yao iliyozinduliwa rasmi leo June 22, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 22, 2015

SIMBA SPORTS CLUB:-Ifahamu Tovuti yao iliyozinduliwa rasmi leo June 22, 2015.

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Tovuti ya klabu hiyo www.simbasports.co.tz jijini Dar es Salaam. Wengine ni Makamu wa rais, Geofrey Nyange Kaburu (kushoto waliosimama) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAG group, Imani Kajula ambaye ni  washauri watekerezaji wa Biashara na Masoko wa Simba. (Picha na Tovuti ya Simba SC).

 Simba Sports Club leo June 22, 2015 hii imezindua tovuti yake Ili kukuza mawasiliano na wadau wake mbalimbali hususani; wanachama, wapenzi, vyombo vya habari na wadau wengine muhimu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika dunia na zama za utandawazi tovuti ndio na mitandao ya jamii ndio njia kuu ya mawasiliano. Sisi tuliliona hili na leo hii nafurahi kuwa Simba Sports Club itazindua rasmi tovuti yake ambayo itakuwa jukwaa kuu la mawasiliano na utoaji wa taarifa za klabu ya Simba. Natarajia wengi wenu mtaitumia kikamilifu na muhimu zaidi mtatupa mrejesho chanya kuhusu tovuti yetu’’.
Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Simba www.simbasports.co.tz pamoja na kutangaza ujio wa kocha mpya atakayeinoa timu hiyo, Dylan Kerr raia wa Malta.

Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula na Mtaalamu wa IT, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Robert Lazaro.

Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Simba www.simbasports.co.tz pamoja na kutangaza ujio wa kocha mpya atakayeinoa timu hiyo, Dylan Kerr raia wa Malta. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula na kulia ni Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' 

Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba alisema ‘’ Tovuti hii sio tu itaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbali bali pia itatumika kwa ajili ya uuzaji wa vifaa vya Simba, Bidhaa mbalimbali mpya na muhimu zaidi kuwaunganisha wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kutumia mitandao ya jamii iliyo rasmi ya Simba Sports Club’’.

Mkutano huo wa wandishi wa habari ulitumika kutaarifu Wanachama, Wapenzi na Vyombo vya habari juu ya kocha mpya wa Simba. 

Alizungumza wakati wa kumtambulisha kocha mpya wa Simba, Rais Aveva alisema ‘’Baada ya kupitia vyeti na maombi ya makocha mbalimbali, Napenda kuwataarifu kuwa Klabu ya Simba imeingia kwenye mkataba wa kuifundisha na kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza. Ni kocha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30, akiwa amefanya kazi Nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza, Scotland, Vietnam na Afrika ya Kusini’’.

Aliendelea kusema ‘’Tunaamini ujuzi na uzoefu wake wa ukocha na pia kama mchezaji wa kiwango cha juu utakuwa chachu ya kuifanya Simba ifanye vizuri’’

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad