KWA MUJIBU
WA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU imetoa makadirio ya idadi ya watu wanaotarajiwa
kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 ambao wanakisiwa kuwa watafikia
milioni 24.2 nchi nzima.
Taarifa hizo
ni makadirio ya idadi ya watu wanaostahili kupiga kura katika majimbo ya
uchaguzi Tanzania kwa mwaka 2015.
Katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, idadi ya wapigakura waliojiandikisha ilikuwa
20,137,303, lakini waliopiga kura Oktoba 31 mwaka huo 2010 walikuwa 8,626,283
sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha.
Takwimu hizi
zimetolewa katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Jimbo la Uchaguzi na Kata au Shehia
kama yalivyokuwa mwaka 2010. Makadirio ya idadi ya wapigakura yametokana na
Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.
Kwa mujibu
wa ripoti iliyo kwenye kitabu maalumu cha takwimu za wapiga kura mwaka huu 2015,
ambayo nakala yake imepatikana kupitia Ofisi ya Takwimu ya Mkoa wa Arusha,
idadi hiyo imepatikana kwa kutumia mbinu za kidemografia zinazohusisha
mabadiliko katika viwango vya uzazi, vifo, uhamaji na uhamiaji katika ngazi ya
Taifa, Mkoa, Wilaya, Majimbo ya Uchaguzi na Kata au Shehia husika.
Inakadiriwa
kuwa ifikapo siku ya uchaguzi,2015, Tanzania itakuwa na watu wapatao 48,522,229
ambapo watakaokuwa na umri wa kupiga kura watakuwa ni watu 24,252,927 iwapo
wote watafanikiwa kuandikishwa upya.
Mkoa wa Dar
es Salaam wenye majimbo nane unatarajiwa kuwa na wapiga kura wengi zaidi watakaofikia
milioni 3, ukifuatiwa na Mbeya itakayokuwa na wapiga kura milioni 1.5, Mwanza
milioni 1.4 na Morogoro itakayokuwa na wapigakura milioni 1.3 katika nafasi ya
nne.
Mikoa
mingine inayotarajiwa kuwa na wapiga kura wengi ni pamoja na Kagera itakayokuwa
na wapigakura milioni 1.2, Tabora inayokadiriwa kuwa na idadi ya wapiga kura
milioni 1.1, Tanga nayo kwa idadi kama hiyo ya milioni 1.1 pamoja na Dodoma
itakayokuwa na wastani wa wapigakura milioni moja.
Mkoa wa
Kilimanjaro unatarajiwa kuwa na wapiga kura 976,000 katika nafasi ya tisa na
hatimaye Arusha kufunga kumi- bora ikiwa na matarajio ya wapiga kura wapatao
944,000.
Idadi ya wapigakura watarajiwa kwa mikoa mingine ni kama ifuatavyo:-
Mara
(834,000),
Geita (808,000),
Ruvuma (783,000),
Mtwara (773,000),
Shinyanga
(762,000),
Manyara (741,000),
Simiyu (714,000),
Singida, (698,000),
Pwani
(644,000),
Iringa (524,000),
Rukwa (472,000)
na Njombe (393,000).
Mkoa mpya wa
Katavi, ambao una idadi ya wakazi wapatao 609,000 ndio utakuwa na idadi ndogo
zaidi ya wapigakura kwa Tanzania bara wakitarajiwa kuwa 271,000.
Huko visiwani
mkoa wa Mjini Magharibi unatarajiwa kuwa na wapigakura 347,000, Kaskazini
Unguja 104,000, Kaskazini Pemba 103,000, Kusini Pemba 95,000 na Kusini Unguja
69,000.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment