LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Matokeo ya leo Februari 21,2015 kwa Chelsea, Arsenal na Manchester United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 21, 2015

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Matokeo ya leo Februari 21,2015 kwa Chelsea, Arsenal na Manchester United.

Swansea 2 - 1 Manchester United.

Kama walivyofanya katika Mechi ya ufunguzi wa Msimu huu 2014/2015 huko Old Trafford Mwezi Agosti, Swansea Leo Februari 21,2015  wakiwa kwao Liberty Stadium wameipiga Man United Bao 2-1.


Man United walitangulia kufunga kwa Bao la Anders Herrera la Dakika ya 28 na Swansea kusawazisha Dakika ya 30 kwa Bao la Ki Sung-yueng na kisha Gomis kuwapa ushindi kwa bao la kibahati baada ya Shuti la Mita 25 la Jonjo Shelvey kumbabatiza usoni na kumhadaa Kipa David de Gea.   

Chelsea 1 - 1  Burnley .

Chelsea, wakichezwa kwao Stamford Bridge, wametoka Sare 1-1 na Burnley ambayo inapigana isishushwe Daraja.

Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Branislav Ivanovic la Dakika ya 14 lakini wakawa pungufu katika Dakika ya 70 pale Nemanja Matic alipopewa Kadi Nyekundu alipolipizia Rafu toka kwa Ashley Barnes.

Burnley walisawazisha kwa Bao la Kichwa la Ben Mee kufuatia Kona ya Dakika ya 81.

Crystal Palace 1 - 2 Arsenal.

Penati ya Santi Cazorla na Bao la Olivier Giroud, yote Kipindi cha Kwanza, yamewapa Arsenal wa Ugenini wa Bao 2-1 walipoichapa Crystal Palace na kutwaa Nafasi ya 3 kwa kuishusha Man United Nafasi ya 4.

Bao pekee la Palace lilifungwa Dakika ya 90 na GlennMurray.

LIGI KUU ENGLAND 2014/2015 RATIBA.

Jumapili Februari 22,2015.

1500 Tottenham v West Ham 
    
1705 Everton v Leicester  
          
1915 Southampton v Liverpool 
            
MSIMAMO:

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad