LA LIGA 2014/2015:- Picha Barcelona ikifungwa 0-1 Malaga na kusindwa kuing’oa Real Madrid kileleni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 21, 2015

LA LIGA 2014/2015:- Picha Barcelona ikifungwa 0-1 Malaga na kusindwa kuing’oa Real Madrid kileleni.

FC Bacelona Leo Februari 21,2015 wameikosa nafasi safi sana ya kuiporomosha Real Madrid kutoka kilele cha La Liga walipofungwa kwao Nou Camp Bao 1-0 Malaga.

Bao la ushindi la Malaga lilifungwa Dakika ya 7 tu kufuatia Beki wao Dani Alves kurudisha Pasi fupi kwa Kipa wake Claudio Bravo na Straika wa Malaga, Juan Miguel Jimenez Lopez, kuunasa Mpira huo na kufunga.

Mwezi Septemba 2014, huko kwao La Rosaleda, Malaga ilifanikiwa kutoka 0-0 na Barcelona.

Matokeo haya yamewabakisha Vinara Real Madrid kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 1 mbele na Mechi moja mkononi ambayo watacheza Kesho Jumapili Februari 22,2015 Ugenini na Elche.




Baadae Leo, Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, ambao walichapwa 2-0 na Celta Vigo katika Mechi iliyopita na kubaki wakiwa Nafasi ya 3 Pointi 6 nyuma ya Barcelona, wapo Nyumbani kwao Vicente Calderon kucheza na UD Almeria.

Mechi nyingine hii Leo ni kati ya Cordoba CF na Valencia CF na kumalizia Mechi kati ya Deportivo La Coruna na Celta de Vigo.

LA LIGA RATIBA/MATOKEO.

Ijumaa Februari 20,2015.

Getafe CF 2 - 1 RCD Espanyol 

Jumamosi Februari 21,2015.

FC Barcelona 0 - 1 Malaga CF 

2000 Cordoba CF v Valencia CF

2200 Atletico de Madrid v UD Almeria

0001 Deportivo La Coruna v Celta de Vigo

Jumapili Februari 22,2015.

1400 Real Sociedad v Sevilla FC

1900 Athletic de Bilbao v Rayo Vallecano

2100 Villarreal CF v SD Eibar

2100 Elche CF v Real Madrid CF

Jumatatu  Februari 23,2015.

2245 Levante v Granada CF

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad