EPL 2014/2015:-Manchester City 5-0 Newcastle United,Sasa pointi 5 baada ya Chelsea kutoka sare mechi ya Jana Februari 21,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 22, 2015

EPL 2014/2015:-Manchester City 5-0 Newcastle United,Sasa pointi 5 baada ya Chelsea kutoka sare mechi ya Jana Februari 21,2015.

Mabingwa Manchester City Jana Februari 21,2015,usiku wamapata ushindi wao mkubwa Msimu huu 2014/2015  kwenye Ligi Kuu Uingereza walipoitandika Newcastle United Mabao 5-0 Uwanjani Etihad na kujizatiti kwenye Nafasi ya Pili wakilikata pengo na Vinara Chelsea kuwa Pointi 5 baada ya Vinara hao kutoka Sare 1-1 na Burnley hapo Jana pia.

Man City, wakicheza tena na Kiungo wao mahiri Yaya Toure aliekuwa na Timu yake ya Taifa Ivory Coast Mwezi Januari na mwanzoni mwa Februari pamoja na Mchezaji mpya Wilfried Bony alieanzia Benchi hapo Jana walitawala Mechi hii.

Man City walitangulia kupata Bao kwa Penati ya Dakika ya Pili tu kufuatia makosa ya Anita kuupoteza Mpira na kumchezea Rafu Edin Dzeko na Penati hiyo kufungwa na Sergio Aguero.

Dakika 10 baadae Samir Nasri alipiga Bao la Pili na Dakika ya 21 Edin Dzeko kutia Bao la 3.

Kipindi cha Pili David Silva aliongeza Bao 2 katika Dakika za 51 na 53.


LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015 RATIBA.

Jumapili Februari 22,2015.

1500 Tottenham v West Ham 
    
1705 Everton v Leicester  
          
1915 Southampton v Liverpool 
            
MSIMAMO.

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad