RATIBA EPL 2014/2015:-Januari 10,2015 Sunderland v Liverpool , Chelsea v Newcastle Na Januari 11,2015 Arsenal v Stoke . - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Saturday, January 10, 2015

demo-image

RATIBA EPL 2014/2015:-Januari 10,2015 Sunderland v Liverpool , Chelsea v Newcastle Na Januari 11,2015 Arsenal v Stoke .

.com/simgad/
2489EF4A00000578-2903452-image-a-87_1420812284938
Ligi kuu soka Uingereza 2014/2015 inarejea  dimbani leo hii Jumamosi Januari 10,2015 na Mechi ya utangulizi ni huko Stadium of Light kati ya Wenyeji Sunderland na Liverpool.

Sunderland wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa Nafasi ya 14 na wana Pointi 20 wakati Liverpool wako Nafasi ya 8 na wana Pointi 29.

Nao Chelsea na Man City, ambao wamefungana kwa Pointi wote wakiwa na Pointi 46 kila mmoja na pia idadi sawa ya kila kitu kingine ikiwa ni pamoja na Mechi walizoshinda, kufungwa na sare na pia Magoli ya kufunga na kufungwa.

Chelsea wao watakuwa Nyumbani kwao Stamford Bridge kucheza na Newcastle, Timu ambayo ndio ilikuwa ya kwanza kuifunga Chelsea kwenye Ligi Msimu huu waliposhinda 2-1 katika Mechi ya kwanza huko St James Park mapema Mwezi Desemba.
2489EF4100000578-0-image-a-62_1420811027964
Mabingwa Watetezi Man City wao watakuwa Ugenini huko Goodison Park kwa kucheza na Everton ambao Msimu huu wanasuasua na wapo Nafasi ya 13 wakiwa Pointi 25 nyuma ya City.

Mechi ya mwisho kwa Jumamosi ni ile ya Crystal Palace, ambao watakuwa Nyumbani Selhurtst Park, kucheza na Tottenham Hotspur.

Jumapili Januari 11,2015,kutakuwa na  Mechi mbili na ya kwanza ni huko Emirates ambapo Arsenal, walio Nafasi ya 6, wakiikariribisha Stoke City ambao wako Nafasi ya 11.

Mechi ya mwisho Siku hiyo ya Jumapili ni Uwanjani Old Trafford wakati Timu ya 3 Manchester United watakapokuwa Wenyeji wa Timu ya 4 Southampton ambao wako Pointi 1 tu nyuma ya Man United.

MSIMAMO EPL 2014/2015.
BPL-TEBOJAN1B
RATIBA**Saa za Bongo.

Jumamosi Januari 10,2015.

1545 Sunderland v Liverpool     
           
1800 Burnley v QPR    
     
1800 Chelsea v Newcastle    
      
1800 Everton v Man City     
       
1800 Leicester v Aston Villa   
              
1800 Swansea v West Ham   
               
1800 West Brom v Hull   
           
2030 Crystal Palace v Tottenham

Jumapili Januari 12,2015.

1630 Arsenal v Stoke     
            
1900 Man United v Southampton

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *