LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Tazama Stand United ilivyoisimamisha Simba SC Taifa Leo Oktoba 04,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 04, 2014

LIGI KUU VODACOM 2014/2015:-Tazama Stand United ilivyoisimamisha Simba SC Taifa Leo Oktoba 04,2014.

Kipa wa timu ya Stend United, John Mwenda akiukodolea macho mpira uliopigwa na Shaban Kisiga ukiingia wavuni wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika Uwanja wa Taifa Leo Oktoba 04,2014.

 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba imetoka 1-1 na Stand United ya Shinyanga. Bao la Simba limefungwa na Shaaban Kisiga la Stand limefungwa na Kheri Mohammed.

Wachezaji wa Simba wakishangilia goli lao.....Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo Oktoba 04,2014, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wenyeji Polisi wametoka sare ya 1-1 na Kagera Sugar.
 
Polisi walitangulia kupata bao kupitia kwa Nicholas Kabipe dakika ya tano, kabla ya Rashid Mandawa kuisawazishia Kagera dakika ya 88.
 
Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wenyeji Ruvu Shooting wametoka sare ya 0-0 na Mbeya City, wakati Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Coastal Union wameshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.

Mabao ya Coastal yamefungwa na Joseph Mahundi dakika ya kwanza na Hussein Swedi dakika ya 26, wakati la Ndanda limefungwa na Nassor kapama dakika ya 57.







Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya leo Oktabo 04,2014.

Kwa sare hiyo, Azam FC inatimiza pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na kushinda mbili- hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi sita.
 
Mtibwa Sugar watacheza kesho Oktoba 05,2014 na Mgambo JKT ya Tanga Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro mchezo ambao wakishinda watapaa kileleni.

Simba SC 1-1 Stand Utd

Coastal Unioni 2-1 Ndanda FC

Polisi 1-1 Kagera Sugar

Prisons 0-0 Azam FC

Ruvu Shoot 0-0 Mbeya City

Kesho-Oktoba 05,2014.

Yanga SC Vs JKT Ruvu

Mtibwa Sugar Vs Mgambo 

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
  


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad