Ukitaka kujua kuwa ku-shine hapa Bongo ni juhudi zako tu mwenyewe za
kupiga kazi usiku na mchana bila kulala na mwisho wa siku kufikia malengo yako
basi mfano wa kuigwa ni huyu Birthday boy Diamond Platnumz.
Diamond alizaliwa tarehe 02, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana
Dar es salaam mnamo wa saa kumi na moja na kupewa jina la
Nasibu Abdul Juma .
Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila
msaada wowote na ikabidi wahamie Tandale Magharibi kwa bibi
yake mzaa mama, na hapo ndipo yakawa makazi yao.
Historia yake ni ya kusikitisha kama alivyoelezea kwenye wimbo wa
binadamu wabaya.
Mnamo mwaka 1995 alianza kupata elimu ya Nursery katika shule ya
Chakula Bora iliyopo Tandale Uzuri hadi alipomaliza na kujiunga na Elimu
ya Msingi yaani (Primary School) mwaka 1996 katika shule ya msingi
Tandale magharibi iliyopo jijin Dar-es-salaam.
Ilipofika mwaka 2000 akiwa darasa la tano diamond alionekana kuanza
kupenda sana muziki, hivyo alianza kucopy baadhi ya na kukrem nyimbo
za wasanii waliokuwa wakihit ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho na
kuwa anaimba katika sehem tofautitofauti.
|
No comments:
Post a Comment