LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:- Haya hapa matokeo ya Liverpool dhidi ya West Brom ,Kesho ni Chelsea v Arsenal.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 04, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:- Haya hapa matokeo ya Liverpool dhidi ya West Brom ,Kesho ni Chelsea v Arsenal..

Liverpool leo Octoba 04,2014,jioni imepata ahueni na bila shaka kocha Brenden Rodgers atapumua leo. Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 2-1 West Bromwich Albion Uwanja wa Anfield.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Adam Lalana dakika ya 45 na Jordan Henderson dakika ya 61, wakati bao pekee la WBA lilifungwa na Saido Berahino kwa penalti dakika ya 56.

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu ya England jioni ya leo Octoba 04,2014, Hull City imeifunga 2-0 Crystal Palace, mabao ya Mohamed Diame dakika ya 61 na Nikica Jelavic dakika ya 89.

Leicester City imetoka 2-2 na Burnley. Mabao ya Leicester yamefungwa na Jeffrey Schlupp dakika ya 34 na Riyad Mahrez dakika ya 41, wakati ya Burnley yamefungwa na Michael Kightly dakika ya 39 na Ross Walace dakika ya 90.

Swansea City imetoka sare ya 2-2 na Newcastle United, mabao yake yakifungwa na Wilfried Bonny dakika ya 17 na Routledge dakika ya 50, huku ya wapinzani wao yakifungwa na Papiss Cisse dakika ya 43 na 75.

Sundeland imeichapa 3-1 Stoke City, mabao yake yakitiwa kimiani na Cannor Wickham dakika ya nne, Steven Fletcher dakika ya 23 na 79, wakati bao la kufutia machozi la wapinzani wao limefungwa na Charlie Adam dakika ya 15.  
Hapo kesho JUMAPILI Octoba 05,2014,Uwanjani Stamford Bridge Wenyeji Chelsea watapambana na Arsenal katika mtanange mkali wa Ligi Kuu .

Mechi hiyo ina chachu kubwa huku Chelsea wakiwa kileleni mwa Ligi wakiwa wameshinda Mechi 5 na Sare moja na wako Pointi 6 mbele ya Arsenal ambao wako Nafasi ya 4 wakiwa wameshinda Mechi 2 na Sare 4.

 Jumapili Oktoba 5,2014.

1400 Man United v Everton

1605 Chelsea v Arsenal

1605 Tottenham v Southampton

1815 West Ham v QPR
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad