Tazama Picha 31 za Jinsi matembezi yahisani ya km 29 kutoka Ofisi za Radio Kwizera hadi kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera yalivyofanikiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 24, 2013

Tazama Picha 31 za Jinsi matembezi yahisani ya km 29 kutoka Ofisi za Radio Kwizera hadi kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera yalivyofanikiwa.

Matembezi hayo ya Hisani  ya km 29  yamefanyika Desemba 21,2013 na yalikuwa na Lengo la Kuhamasisha Amani,Usalama,Maendeleo na Ushirikiano ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Masawe(mwenye trakisuti ya orenji) alihudhuria pia matembezi hayo kwa kutembea kutoka Ofisi za Radio Kwizera (Mjini Ngara )hadi kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera yalivyofanikiwa.

Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ngara ,Costantine Kanyasu akisaini kitabu cha wageni huku kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera ,Fabian Masawe-wakati walipowasili katika Ofisi za Radio Kwizera Mjini Ngara.

Wana matembezi kutoka taasisi mbalimbali,mshirika na watu binafsi wakijiandaa kwa kuanza matembezi hayo ya km 29,matembezi yaliyoanzia  Ofisi za Radio Kwizera Mjini Ngara hadi (Hotel ya Tumaini Letu)Kabanga.
Matembezi yakiwa yamepamba moto..........Mkuu wa Mkoa wa Kagera ,Fabian Masawe,sambamba na mwenyeji wake Costantine Kanyasu(Mkuu wa wilaya ya Ngara)Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngara John Shimilimana,Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Ngara Julius Nestory pamoja na wadau wengine.
Kutoka katikati ni Afisa Michezo wilaya ya Ngara Saidi Salumu,kulia kwake ni Kaimu Fundi mkuu Idara ya Ufundi Radio Kwizera Yohana Bitta wakiendelea na matembezi ya hisani ya km 29 kuelekea Mjini Kabanga.
Hapa ndipo wana matembezi walipomalizia matembezi yao ya km 29 katika Hotel ya Tumaini Letu-Mjini Kabanga.
Pamoja na mambo mengine wanamatembezi walipata kufahamiana kwa kujitambulisha kisha kunywa ,kula na kucheza muziki ikiwa ni ishara ya kufurahi pamoja.
Chears pia ziligongwa .........
Mmiliki wa Blog hii ya (mwanawamakonda) nae hakuwa nyuma katika matembezi hayo ya hisani ya km 29 katika kuhamasisha Amani,Usalama,Maendeleo na Mshikamano.
Wanamatembezi wakipata chakula  ndani ya ukumbi wa nje wa Hotel ya Tumaini Letu...........
Muziki ulifunguliwa........kisha wanamatembezi wakaanza kuyarudi masebene na kusahau umbali wa km 29 walizotembea toka  Ofisi za Radio Kwizera Mjini Ngara hadi Kabanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad