Tazama Picha 13 za Miradi ya Maendeleo wilayani Ngara iliyokaguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Fabian Masawe(Mulokozi). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 22, 2013

Tazama Picha 13 za Miradi ya Maendeleo wilayani Ngara iliyokaguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Fabian Masawe(Mulokozi).



Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Kanali mstaafu Fabiani Masawe jana (Desemba 21,2013)amefanya ziara ya siku moja wilayani Ngara mkoani humo, kukagua miradi ya maendeleo hasa ya Ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, miradi ya maji (Tarafa ya Rulenge) pamoja na kuhamasisha wananchi kujitolea kuweka ushiriki wao katika kuikamilisha na kuilinda ili kuwa endelevu.



Mkuu wa mkoa wa Kagera ,Kanali mstaafu Fabiani Masawe (Mulokozi) akitazama maji safi na salama alipokagua mradi huo wa maji katika tarafa ya rulenge wilayani Ngara pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi  kuilinda pamoja na kuifanya ukarabati  pale inapochakaa kwa kuwa inawaletea manufaa(Nyuma yake ni MNEC Issa Samma na Mwenye miwani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu).

Baadhi ya wadau wa maendeleo wakinawa  maji safi na salama katika moja ya mradi wa maji  katika tarafa ya rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.




Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw Julius Nestori amesema ujenzi wa maabara na miundombinu mbalimbali  na miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600,inajengwa kwa ufadhili wa benki ya dunia.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad