Hivi ndivyo Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro walivyokamata gari lenye Maiti yenye Madawa ya Kulevya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 26, 2013

Hivi ndivyo Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro walivyokamata gari lenye Maiti yenye Madawa ya Kulevya.

Hizi ndio baadhi ya Pipi zilitolewa tumboni mwa Marehemu Khalid Kitala (47) na
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari  hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Baadhi ya Makachero wa Polisi wakijadiliana jambo baada ya kuona Mwili huo.ukikamatwa kwenye  gari dogo aina ya Toyota Spacio.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro,Faustine Shilogile akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).


Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya Toyota Spacio likiwa limebeba mwili wa mtu aliefariki ambaye alitambulikwa kwa Jila la Khalid Kitala (47) na kukutwa na kete kadhaa za Madawa ya Kulevywa tumboni.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa walipata taarifa za kuwepo kwa gari  hilo toka kwa wasamalia wema ambao waliliona njiani, ambapo inasemekana lilikuwa linatokea Mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Polisi wa mkoa wa Morogoro waliweka  mtego wao kwenye kituo cha Mikumi na hatimaye kufanikiwa kukamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa),pipi saba za vitu vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.

Mwili huo ulipelekwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na pipi nyingine kumi na saba tumboni mwa Marehmu huyo na inasemekana mtu huyo alifariki akiwa Mbeya.

Watu wote watatu ambapo wawili wanahusika na gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara wa Kariakoo wanashikiliwa na polisi huko Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad