![]() |
Mchango wako
wa hali na mali unahitajika ili kumsaidia Matibabu Mtoto Siwema miaka 12 Baada
ya kulipukiwa na Bomu :-CHANGIA KUPITIA
M-PESA 0753714845.
|
Mototo Siwema Chiza mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa
kijiji cha Mumilamila Kata ya Bugarama
wilayani Ngara mkoani Kagera, na pia
ni Mwanafunzi wa Darasa la tano shule ya msingi Mumilamila yuko katika wakati mgumu yeye na familia yake
baada ya mtoto huyo wa kiume mnamo tarehe 11 mwezi October mwaka huu (2013) kulipukiwa
na bomu katika kijiji hicho.
Mtoto
huyo anaye lelewa na baba yake pekee
na baba akiwa hana uwezo kifedha alikumbwa
na mkasa huo wa kulipukiwa na bomu wakati akiwa na kaka yake wakielekea
shambani kwao.
Bom hilo
lilimuaribu sana mototo huyo sehemu ya tumbo na miguu yake na tunaishukuru Hospitali ya Rulenge kwa
ujuzi wao waliweza kumfanyia upasuaji wa utumbo na kumtibu mtoto huyo sehem za tumbo ikiwa ni sehemu ya kwanza ya matibabu.
Mpaka sasa
tatizo limebaki katika sehemu ya miguuni
ambapo Hospitali ya Rulenge kutokana ukosefu wa vifaa wameshindwa
kumtibu mtoto huyo (Siwema) ambapo sasa
amepewa rufaa kwa ajili ya upasuaji mkubwa katika sehem za miguu ambapo kwa sasa yuko
katika Hospitali ya Murugwanza katika wodi ya majeruhi akiendelea kutibiwa.
Kwa Mujibu
wa Daktari anaemtibu katika Hospitali ya
Murugwanza amesema mtoto huyo anaendelea vizuri ila anahitaji kufanyiwa
upasuaji mkubwa katika miguu yake iliyoathiriwa na bomu hilo ambapo Hospitali
hiyo imempa rufaa ya kwenda Hospitali ya Bugando Jijini Mwanza ili aende
akatibiwe.
Kikwazo
kikubwa ni gharama za matibabu hayo ambapo
baba yake mzazi hana uwezo wa kifedha na bado pia katika Hospitali ya Rulenge na
Murugwanza bado kuna deni lakini pia kwenda hospitali ya Bugando -Mwanza wanahitaji
gharama ya kumtibu …. chakula na mahitaji mengine hivyo mtoto huyu yuko katika
wakati mgum.
Mchango wako
wa hali na mali unahitajika ili kumsaidia Matibabu Mtoto Siwema miaka 12 Baada
ya kulipukiwa na Bomu :-CHANGIA KUPITIA
M-PESA 0753714845.
No comments:
Post a Comment