Mchezaji Philip
Lahm (katikati) alifunga bao la kwanza la Bayern Munich wakati FC Barcelona wakifungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki
mjini Munich hapo jana usiku (Julai 24,2013).
|
Kocha Mpya
wa Bayern Munich, Pep Guardiola ameifunga timu yake ya zamani, FC Barcelona
mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki mjini Munich hapo jana usiku (Julai
24,2013).
|
Goli la Pili
la mchezaji Mario Mandzukic wakati Bayan Munich ilipoiburuza FC Barcelona mabao 2-0 katika mchezo huo wa kirafiki mjini Munich hapo
jana usiku (Julai 24,2013).
|
Wachezaji Thiago
(kushoto) na Boateng (kulia) wa Bayan Munich wakimdhibiti Nahodha wa FC Barcelona, Lionel
Messi katika mchezo huo wa kirafiki mjini Munich hapo jana usiku (Julai
24,2013).
|
Frank Ribery
akipambana na Marc wa FC Barcelona katika
mchezo huo wa kirafiki mjini Munich hapo jana usiku (Julai 24,2013).
|
Kocha Mpya
wa Bayern Munich, Pep Guardiola ameifunga timu yake ya zamani, FC Barcelona
mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki mjini Munich hapo jana usiku (Julai
24,2013).
Katika
Mchezo huo wa Ziara, FC Barcelona iliyokuwa bila Kocha wao mpya Gerardo Martino
na pia Mchezaji mpya Neymar na mihimili yao, Xavi na Andres Iniesta, Pep
Guardiola alitumia Mfumo mpya kwa Bayern wa kutokuwa na Straika anaetambulika
huku akimchezesha Kepteni wao, Philipp Lahm, ambae amezoeleka kama Fulbeki wa
kulia, kama Kiungo Mshambuliaji huku nyuma yake akiwepo Kiungo wao mpya Thiago
Alcantara.
Mchezaji Philipp
Lahm alifunga bao la kwanza dakika ya 14 na timu zikaenda kupumzika matokeo ya
1-0, kabla ya Bayern kupata bao la pili dakika ya 87 lililofungwa Mario
Mandzukic.
Kikosi cha
Bayern Munich kilikuwa: Neuer/Starke dk46, Rafinha, Dante/Van Buyten dk59,
Boateng, Alaba, Thiago, Lahm/Gustavo dk59, Kroos, Ribery, Robben/Shaqiri dk46
na Muller/Mandzukic dk46.
FC Barcelona: Pinto/Oier
dk46, Montoya/Kiko dk46, Bartra/Gomez dk46, Mascherano/Planas dk46, Adriano/Patric
dk46, Song/Espinosa dk46, Sergi Roberto/Ilie dk46, Dos Santos/Quintilla dk46,
Tello/Joan Roman dk46, Messi/Dongou dk46 na Alexis/Dani Nieto dk46.
No comments:
Post a Comment