Hivi ndivyo Rais wa Tanzania ,Dr.Jakaya Kikwete alivyoweka Jiwe la Msingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba,Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 24, 2013

Hivi ndivyo Rais wa Tanzania ,Dr.Jakaya Kikwete alivyoweka Jiwe la Msingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba,Mkoani Kagera.

 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete  akivishwa bendera ya skauti mara baada ya  kuwasili uwanja wa ndege wa Bukoba leo (Julai 24,2013) kuanza ziara ya Kikazi Mkoani Kagera na Kushiriki Siku ya Mashujaa Kitaifa Mkoani humo,Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa kagera Kanali Mstaafu Fabian Masawe.

Rais Kikwete akihutubia Wananchi uwanjani hapo ambapo pamoja na mambo mengi , Uwanja huo upo katika hatua ya kwanza kukamilika ambapo zinaruka na kutua ndege mbalimbali, lakini rais ameahidi kutengeneza uwanja mwingine wa kimataifa wilayani misenyi wa Omukajunguti.

 Rais  Kikwete akipewa taarifa na kusomewa ramani na mtaalamu wa ujenzi wa uwanja wa ndege  wa  Bukoba mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera  leo (Julai 24,2013) kuanza ziara ya Kikazi  Mkoani Kagera na Kushiriki Siku ya Mashujaa Kitaifa Mkoani humo.

  Rais Kikwete akielekea kufungua pazia ya jiwe la msingi la  ujenzi wa uwanja wa ndege  wa  Bukoba baada ya kukata utepe mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera  leo (Julai 24,2013) kuanza ziara ya Kikazi  Mkoani Kagera na Kushiriki Siku ya Mashujaa Kitaifa Mkoani humo.

Baadhi ya Muonekano wa sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Rais Kikwete akisalimiana na Baba Askofu Kilaini alipowasili uwanja wa ndege wa Bukoba leo (Julai 24,2013) kuanza ziara Mkoani Kagera na Kushiriki Siku ya Mashujaa Kitaifa Mkoani humo.

Hapa Rais Kikwete akihutubia wananchi baada ya kuzindua jengo la cha acha ushirika Kagera KCU.

Ni picha ya pamoja na viongozi wa ushirika nyuma jengo hilo lililozinduliwa linaonekana kwa mbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad