Rais Kikwete awasili Mkoani Kagera tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita pamoja na kuongoza kumbukumbu za mashujaa wa Kagera leo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 25, 2013

Rais Kikwete awasili Mkoani Kagera tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita pamoja na kuongoza kumbukumbu za mashujaa wa Kagera leo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Mstaafu Fabia Massawe baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013) tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo.



Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman ambaye pia yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.


Rais Kikwete akisalimiana na Mstahiki Meya wa Bukoba Mhe Anatory Amani.


Vijana wa Skauti wa Bukoba wakimlaki Rais Kikwete  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013) tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo.


Kijana wa Skauti akipiga saluti kuomba kumvisha skafu Rais Kikwete.


Rais Kikwete akivishwa skafu.


Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli. Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe.


Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.


Rais Kikwete akisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kagera waliofika uwanjani kumlaki.


Rais Kikwete akisalimiana na Mkuu wa JKT.


Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mbalimbali Mkoani Kagera waliokuwepo uwanjani hapo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013) tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo.


Rais Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013) tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo.


Ngoma ya Kihaya ikimlaki Rais Kikwete  mjini Bukoba mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013) tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo.


Sehemu ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013).


Viongozi wa dini Mkoani Kagera wakiwa bega kwa bega kwenye sherehe hizo za kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba jana(Julai 24,2013).


Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akimkaribisha Rais Kikwete kuongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.


Rais Kikwete akiongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.


Rais Kikwete akipata maelezo kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.


Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka  jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba jana (Julai 24,2013).


Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe Peter Serukamba wakishangilia wakati Rais Kikwete akiweka jiwe la msingi jana(Julai 24,2013) katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.


Hapa Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.


Rais Kikwete akisalimiana na Mhashamu Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba.


Sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba unaokarabatiwa na kupanuliwa kwa Hivi sasa ukionekana.


Baada ya Shughuli za Uwanjani ,Rais Kikwete aliwasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd) mjini Bukoba Pia.


Rais Kikwete akisalimiana na wanachama wa KCU alipowasili jana (Julai 24,2013)Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd).


Rais Kikwete akisalimiana na wananchi wa Mjini wa Bukoba waliofurika kushuhudia ufunguzi wa  jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd).


Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD,Bw. John Binushu  akimkaribisha Rais Kikwete Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd) hapo jana(Julai 24,2013).


Sehemu ya umati wa wananchi kwenye ufunguzi wa jengo hilo.


Ni muonekano wa Jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd) lililopo mjini Bukoba.


Rais Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD ,Bw.John Binushu huku Pembeni yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw.Fabian Masawe.


Rais Kikwete akipokea zawadi ya kahawa toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD ,Bw.John Binushu.


Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya Kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd) hapo Jana (Julai 24,2013).


Rais Kikwete akihutubia wananchi baada ya Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd).


Rais Kikwete akihutubia wananchi baada ya Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd).


Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa KCU baada ya kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd).


Rais  wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewasili  Mjini Bukoba tayari kushiriki katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa inayofanyika kitaifa Mkoani KAGERA leo(Julai 25,2013).

 

Mashujaa wa Tanzania waliopigana Vita vya Kagera, wanakumbukwa leo(Julai 25,2013) katika kilele cha sherehe hizo zitakazofanyika kwenye Kambi ya Kaboya mkoani Kagera.




Kwa Mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe amesema  kuwa maandalizi yote yamekamilika na Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo itakayoambatana na uwekaji wa mashada ya maua kuwakumbuka mashujaa hao. 



Mashujaa wa Tanzania wanakumbukwa leo baada ya kumpiga Fashisti Nduli Idd Amin, wakati wa Vita vya Kagera vilivyopiganwa mwaka 1978 na 1979.




Katika mapambano hayo, wapiganaji wa Tanzania wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliyachakaza majeshi ya Nduli Amini wa Uganda.




Mbali na hayo, Rais Kikwete anatarajiwa kuzindua Wilaya mpya ya Kyerwa iliyomegwa kutoka Wilaya ya Karagwe,Kivuko cha Rusumo wilayani Ngara  pamoja na kuzindua mradi wa kuzalisha umeme wa Kaishozi.




Awali maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania yalikuwa yakifanyika kila Septemba Mosi, lakini tarehe hiyo ilibadilishwa na kuwa Julai 25 kwa kuwa ndiyo tarehe waliyopokewa mashujaa hao waliopigana vita vya Kagera.




Hii ni mara ya pili kwa Mkoa wa Kagera kuandaa sherehe hizo ambapo  Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009.




Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein na baadhi ya mawaziri akiwamo, Prof Anna Tibaijuka (Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Harisson Mwakyembe (Uchukuzi), Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Sospeter Muhongo (Nishati na Madini), John Maghufuli (Ujenzi), Mathias Chikawe (Katiba na Sheria), Tersa Huvisa (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira) ni miongoni mwa viongozi wanaoshiriki sherehe hizo.




Baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Bukoba , Rais Kikwete ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.




Katika hotuba yake fupi kabla ya kuweka jiwe la Msingi Rais Kikwete, Amesema ametimiza ahadi yake kwa kukarabati ujenzi wa uwanja huo.




Awali Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali itaendelea na kazi ya kujenga viwanja vya ndege katika baadhi ya mikoa hapa nchini.




Mradi wa ukarabati wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni  21 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania.

Mradi huo ulioanza February 2012 unatarajiwa kumalizika February  2014.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad