Serikali yatoa wiki mbili kwa Wahamiaji Haramu na Majambazi yanayoteka magari na kufanya uvamizi katika Mikoa ya Kagera na Kigoma Kujisalimisha haraka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 26, 2013

Serikali yatoa wiki mbili kwa Wahamiaji Haramu na Majambazi yanayoteka magari na kufanya uvamizi katika Mikoa ya Kagera na Kigoma Kujisalimisha haraka.

Rais wa Tanzania  Jakaya Kikwete akiwa katika ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera leo (Julai 26,2013) amezindua  barabara yenye kiwango cha Lami ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera yenye urefu wa kilometa 200 ambayo imekamilika kwa 97%  ambapo sehemu iliyobaki ni mita 500 na itakamili mwishoni mwa mwezi ujao.

Muonekano wa  barabara yenye kiwango cha Lami ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera yenye urefu wa kilometa 200 ambayo imekamilika kwa 97%  ambapo sehemu iliyobaki ni mita 500 na itakamili mwishoni mwa mwezi ujao.

Rais wa Tanzania  Jakaya Kikwete akiwasili Wilayani Biharamulo mkoani Kagera kuendelea na ziara yake ya siku 6 mkoani humo ambapo akiwa wilayani humo  leo (Julai 26,2013) amezindua  barabara yenye kiwango cha Lami ya Kagoma-Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera yenye urefu wa kilometa 200.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr.Jakaya Kikwete akiwa jukwaa kuu pamoja na Waziri wa Ujenzi Dr.John Pombe Magufuri na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanal mstaafu Fabian Masawe wakati walipo wasili Wilayani Biharamulo mkoani Kagera kuendelea na ziara yake ya siku 6 mkoani humo ambapo akiwa wilayani humo  leo (Julai 26,2013) amezindua barabara ya Lusahunga-Kagoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr.Jakaya Kikwete  mara baada ya uzinduzi wa barabara ,aliwahutubia  Wananchi na Kutoa wiki mbili kuanzia sasa wanaomiliki silaha kinyume cha sharia kuzisalimisha haraka iwezekanavyo sambamba na kuanza  msako mkali kwa majambazi yanayoteka magari na uvamizi mbalimbali katika Mikoa ya Kagera na Kigoma kujisalimisha  na kwamba baada ya hapo Majeshi yote nchini yanaanza msako na wanawahusika hawatakamatwa mateka.


Katikati Ni Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Philip Kalangi  akifuatilia hali ya Ulinzi na Usalama wakati wa uzinduzi  wa barabara ya Lusahunga-Kagoma wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo(Julai 26,2013).




Wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia  uzinduzi  wa barabara ya Lusahunga-Kagoma wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo(Julai 26,2013).



Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli akipinga ngoma ya Nyamigogo wakati wa uzinduzi  wa barabara ya Lusahunga-Kagoma wilayani Biharamulo mkoani Kagera leo(Julai 26,2013).

Baada ya Uzinduzi wa Barabara hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr.Jakaya Kikwete  amepanda mti  katika eneo la uzinduzi huliofanyika eneo la Njia panda wilayani biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya Serikali kuhamasisha upandaji miti na utunzaji Mazingira hapa nchini.

Pia Mawaziri aliombatana nao Waziri wa TAMISEMI Bi.Hawa Ghasia nae alishiriki zoezi la upandaji  mti  katika eneo la uzinduzi huliofanyika eneo la Njia panda wilayani biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya Serikali kuhamasisha upandaji miti na utunzaji Mazingira hapa nchini.


Baada ya Uzinduzi wa Barabara hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr.Jakaya Kikwete  amepanda mti  katika eneo la uzinduzi huliofanyika eneo la Njia panda wilayani biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya Serikali kuhamasisha upandaji miti na utunzaji Mazingira hapa nchini.
Rais Kikwete ambaye anaendelea na ziara yake ya siku 6 mkoani Kagera baada ya Kuzindua barabara ya Lusahunga –Kagoma wilayani Biharamulo,Leo pia(Julai 26,2013) ameendelea na ziara yake  wilayani Ngara  ambapo amehutubia Wananchi wa Rulenge na Ngara Mjini na kusisitiza Suala la Wahamiaji haramu kuondoka haraka nchini pamoja na na Kutoa wiki mbili kuanzia sasa  kwa wanaomiliki silaha kinyume cha sharia kuzisalimisha haraka iwezekanavyo.

Pia Rais Kikwete amesema Serikali itaanza   msako mkali kwa majambazi  yanayoteka magari na kufanya uvamizi mbalimbali katika Mikoa ya Kagera na Kigoma ili kurejesha hali ya usalama katika mikoa hiyo.

Aidha Raisi Kikwete katika ziara hiyo mkoani Kagera ameambatana pia na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe , Profesa Anna Tibaijuka (Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi),Bi. Hawa Ghasia (Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI).

Mawaziri hao kila mmoja kwa nafasi yake walilazimika kujibu Hoja na Kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wabunge kwa Niaba ya Wananchi wao katika sekta ya Maji,Umeme,Barabara,Ardhi pamoja na Kero za Uongozi katika Halmashauri ambapo wameahidi kuzifanyia kazi ili kusukuma mbele maendeleo ya wananchi mkoani Kagera.

Aidha Rais Kikwete ataendelea na ziara yake kesho(Julai 27,2013) kwa kuzindua Kivuko cha Rusumo wilayani Ngara ,kasha kuelekea wilayani Karagwe na hatimae kumaliza ziara yake ya Kikazi mkoani Kagera .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad