Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha
wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.
|
Katika hatua
nyingine, Rais Kikwete amewaahidi Wananchi wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera
kupima ardhi na Kuondoa Mgogoro kutokana na Kupakana na Kambi ya Kaboya.
Hatua hiyo
imekuja baada ya mbunge wa jimbo la Muleba kaskazini
CHARLES MWIJAGE, kumtajia rais mambo yanayowasumbua wananchi wa jimbo
hilo, alipotakiwa na rais kutaja matatizo yanayowakabili wananchi wilayani humo.
Mheshimiwa
Mwijage, amesema kuwa mgogoro wa wananchi na kambi ya Kaboya, aueleweki
kutokana na kutokuwapo mipaka ya kambi hiyo, kitendo kinachosababisha wananchi
washindwe kutumia ardhi kutokana na masuala ya ulinzi na usalama, ilhali jeshi
nalo linatakiwa kuheshimia.
Aidha mbunge huyo amesema kuwa wananchi wakabiliwa
na ukosefu wa huduma ya umeme, ambapo walishapewa ahadi ya kupatiwa huduma hiyo
kupitia REA, lakini hadi sasa hakuna kilichoishatekelezwa na kusababisha lawama
kwa viongozi wa jimbo hilo.
Rais Kikwete
ameendelea na ziara yake mkoani Kagera, ambapo sasa yupo wilayani Muleba ambapo
atahutubia wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo la IYAKO, na
bada ya hapo anapumzika na kuelekea wilayani Biharamulo na Ngara mkoani Kagera
ambako akiwa wilayani Ngara atazindua Kivuko cha Rusumo pamoja na kufanya
mikutano ya hadhara na Wananchi wa Rulenge na Ngara mjini hapo kesho Ijumaa(Julai
26,2013).
No comments:
Post a Comment