![]() |
Rais Uhuru
Kenyatta akila kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye
sherehe zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.
|
![]() |
Rais Uhuru
Kenyatta akisalimiana na Makamu wake William Ruto.
|
Bw.
Uhuru Kenyatta amewataka wananchi wa taifa hilo kuunganisha mawazo yao kwa
ajili ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili ili kuchochea maendeleo.
Akitoa
hatuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa
katika uwanja wa Kasarani mjini Nairobi kwa ajili ya kuanza rasmi majukumu yake
na makamu wake Bw.William Ruto,Rais Kenyatta amesema kuwa baada ya kumalizika
kwa uchaguzi ulioupa ushindi muungano wa Jubilee, kila Mkenya anapaswa
kulitumikia taifa lake kwa nafasi yake ili kuharakisha maendeleo.
Aidha
amewataka wapinzani wake katika uchaguzi uliopita kuungana naye kufanya kazi
kwa ajili ya Wakenya ili kuboresha hali za maisha ya wananchi wao na kwamba
hatapuuza ushauri kutoka kwa kiongozi yeyote waliyechuana naye katika uchaguzi
huo.
No comments:
Post a Comment