Wakati Uganda itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar, Wachezaji 17 na Daktari wa Eritrea waingia mitini . - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Wednesday, December 05, 2012

demo-image

Wakati Uganda itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar, Wachezaji 17 na Daktari wa Eritrea waingia mitini .

.com/simgad/
1
Uganda
Wachezaji wa Uganda wakimpongeza Geoffrey Kizito (anayetazama kamera amekumbatiana na Kiiza), baada ya kufunga bao kwanza dakika ya nne dhidi ya Ethiopia katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala.



Uganda ilishinda 2-0 bao lingine likifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 60 na kwa ushindi huo, Uganda itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar.



IMG_4232
IMG_4225

Kiiza, Walusimbi, Wasswa wakicheza na Ssentongo.


IMG_4150
Harambee Stars
Katika  Robo Fainali ya kwanza ya Kombe hilo la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini Kampala, Uganda,Timu ya  Kenya(Harambee Starz) ilishinda 1-0 dhidi ya Malawi, bao pekee la Mike Barasa dakika ya 56 na sasa Harambee Stars itamenyana na Zanzibar katika Nusu Fainali keshokutwa.




nusuuu

Wachezaji wa timu ya Kenya na Malawi wakiwania mpiara wakati wa mchezo wa nusu fainali ya mchezo wa Cecafa Challenge 2012 uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole nchini Uganda
 

CECAFA_TUSKER_CUP_2012Katika hatua nyingine Vyombo vya Dola Nchini Uganda na Shirikisho la soka nchini humo FUFA, vinafanya msako mkali kuwatafuta Wachezaji 17 na Daktari wa Timu ya Taifa ya Eritrea ambao wametowekaa toka Hotelini kwao na kuwaacha Wachezaji watano tu na Maofisa wawili kupanda Ndege kurudi kwao mara baada ya kutupwa nje ya CHALENJI CUP inayoendelea huko Kampala, Uganda.
 

Akithibitisha kuyeyuka kwa wenzao, Kocha wa Eritrea, Teklit Negash, amesema: “Hatujui Ndugu zetu wako wapi!”



ERITREA

Wachezaji wa timu ya taifa ya Eritrea,
wana sifa kubwa ya kutorokea nchi za watu,
kiasi cha serikali ya nchi yao kuwawekea
 sheria nguvu ya kuweka fedha za kwao
100,000 kama bondi kabla ya kusafiri.
Eritrea ilitolewa kwenye Michuano ya CHALENJI CUP ambako walikuwa Kundi C baada ya kutoka sare 0-0 na Zanzibar, kufungwa 3-2 na Malawi na 2-0 na Rwanda.



Mwaka 2010, kwenye Michuano ya CECAFA Nchini Tanzania, Wachezaji 13 wa Eritrea waliyeyuka na hatimae kubambwa na kuomba Hifadhi ya Kisiasa na baadae kupelekwa huko Houston, Marekani chini ya Programu ya Wakimbizi.



Sasa hii inakuwa desturi sugu ya nchi hiyo kuzamia nchi za watu wanapokwenda kwenye mashindano, kwani awali wachezaji wanne walizamia walipokwenda kucheza na Tusker nchini Kenya kwenye Ligi ya Mabingwa mwaka 2006 mjini Nairobi na wengine zaidi Waliwahi kuzamia pia walipokwenda Angola mwaka 2007 kucheza mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.


IMG_3586
Timu hiyo ilifanya hivyo hivyo mwaka 2009 nchini Kenya na katika kambi nzima alibaki kocha na mchezaji mmoja tu. Kutokana na mfululizo wa matukio hayo, walijitoa kwenye mashindano ya kimataifa mwaka 2010 na mashindano ya mwaka huu ya Challenge ndio ya kwanza kushiriki baada ya kurudi.


Serikali ya Eritrea ilisema ili kudhibiti tabia hiyo, kila mchezaji atatakiwa kuweka bondi fedha za nchi hiyo 100,000 kabla ya kusafiri kwenda kuiwakilisha nchi, lakini hiyo nayo inaonekana bado haijawa tiba.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *