
Inawezekana kukawa na wale ambao wana
sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao
kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au
udhaifu huo.
Wakati
mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa
nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro
fulani waliyo nayo.
Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana
hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado
wao wana sura na miguu au miili mizuri.
Udhaifu
wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya
ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya
mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.

Hebu
angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa.
Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa
nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri
sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi
huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi
hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni
kimbilio la udhaifu wao.
Imeandikwa: MZEE WA UTAMBUZI.
No comments:
Post a Comment