![]() |
Rais
wa Uganda Yoweri Museven
|
Uganda
imeadhimisha miaka hamsini ya uhuru wake huku wakuu kadhaa wa mataifa ya Afrika
wakiungana na Rais Yoweri Museveni katika sherehe hizo mjini Kampala.
Wadadisi
wanasema kuwa Rais Museveni aliyeingia madarakani tangu mwaka 1986 ameiongoza
nchi hiyo kwa kudumisha amani na kuleta maenedeleo baada ya miaka mingi ya vita
vya wenyewe kwa wenyewe na unyanyasaji.
Lakini
wakosoaji wake wanasema amekandamiza upinzani nchini humo.
Kiongozi
wa upinzani Kizza Besigye aliyewekwa kizuizini mara mbili wiki iliyopita
anamshutumu Rais Museveni kwa kuiangamiza nchi hiyo iliyojipatia uhuru wake
toka kwa Waingereza.
Sherehe
za leo zilihuduhuriwa na takriban viongozi 15 wa Afrika wakiwemo marais wa
miaka mingi, Robert Mugabe wa Zimbabwe na Yahya Jammeh wa Gambia.
Rais
Museveni hajasema ikiwa atawania urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2016, ingawa
baadhi ya vigogo katika chama chake wanataka astaafu wakisema kuwa anapoendelea
kusalia mamlakani, ndivyo chama tawala kinaendelea kupoteza ushawishi.
Kwa
wanaharakati wa upinzani ,wasioona cha kusherehekea wanasema kuwa Museveni
amekua mamlakani nusu ya miaka ambayo nchi hiyo imejitawala na hivyo wangetaka
kutumia fursa hiii ya kusherehekea uhuru kumtaka aondoke mamlakani.
Chanzo :BBC.
No comments:
Post a Comment