Serikali
imesema inatambua kwamba Sanaa ni ajira rasmi licha ya kuwa sekta hiyo
inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuratibu, uongozi na kupewa kipaumbele
katika mipango ya kimaendeleo na Serikali.
Akiwasilisha mada ya Umuhimu wa Tasnia ya
Sanaa katika kukuza Ajira nchini, katika Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Sera na
Mipango wa Wizara ya Kazi na Ajira, bwana Haji Janabi amesema sanaa ina mchango
mkubwa katika kukuza na kuendeleza upatikanaji wa nafasi za ajira na kipato.
“Kwa Tanzania iwapo tutatumia vyema uwepo wa
ubunifu muafaka katika sekta ya sanaa zetu bila shaka tasnia hii inaweza
kuchangia sana upatikanaji wa nafasi za ajira na hivyo kuchangia kwa kiasi
kikubwa katika kuondoa tatizo la ajira hapa nchini,” alisema Janabi.
Janabi amesema kwamba pamoja na hivyo kuna
changamoyo kubwa ya kiuratibu na kimuundo ikiwa ni pamoja na Serikali kutotoa
kipaumbe katika masuala yanayohusu sanaa na wasanii pamoja na mgongano wa
kimamlaka kati ya vyombo vinavyohusika na uratibu wa masuala ya sanaa.
Aidha amesema pamoja na nafasi nzuri ya kukuza
ajira, ujio wa teknolojia umeanza kubana soko la ajira ya sanaa ambapo kwa sasa
teknolojia inapunguza uhitaji wa watu katika ufanyikaji wa sanaa kwa akitolea
mfano katika muziki ambapo vitu vingi vinafanywa na mtu mmoja hivyo kupunguza
nafasi za watu wengine.
Pia amesema
ili sekata hii iweze kuwa ajira nzuri zaidi ni muhimu kukaandaliwa viwango na
vigezo kama ilivyo kwa fani zingine ili kuwe na maradaja ya wafanyaji kazi
kulingana na viwango vya umahiri na taaluma.
No comments:
Post a Comment