MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA: [Kila Timu imecheza Mechi 30 v/s UEFA CHAMPIONZ LIGI: Dimbani JUMANNE na JUMATANO - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 27, 2012

MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA: [Kila Timu imecheza Mechi 30 v/s UEFA CHAMPIONZ LIGI: Dimbani JUMANNE na JUMATANO

Manchester United wakiwa Uwanja wa nyumbani Old Trafford kucheza na Fulham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na walipata ushindi wa bao 1-0  kukwea kileleni mwa Ligi na kuipita Man City .


Katika hatua nyingine Mechi za Robo Fainali  za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitachezwa Jumanne na Jumatano huku England ikiwa na mwakilishi mmoja tu, Chelsea, na Spain wakiwa na Timu mbili, Mabingwa watetezi FC Barcelona na Real Madrid.

Timu nyingine ni APOEL Nicosia toka Cyprus, Benfica ya Ureno, Marseille ya Ufaransa, Bayern Munich kutoka Germany na AC Milan ya Italia.

Jumanne kutakuwa na Mechi mbili kati ya APOEL Nicosia v Real Madrid na nyingine ni kati ya Benfica v Chelsea.

Jumatano pia zipo Mechi mbili kati ya Marseille v Bayern Munich na ya pili ni AC Milan v FC Barcelona.

Marudiano ya Robo Fainali hizi ni hapo Aprili 3 na 4 na tayari kila Timu inajua ikiwa itafuzu Robo Fainali nani wanaweza kukumbana nae Nusu Fainali.

NUSU FAINALI

MECHI kuchezwa Aprili 17/18 na Aprili 24/25

Marseille/Bayern Munich v APOELNicosia/Real Madrid

Benfica/ Chelsea v AC Milan/FC Barcelona

FAINALI

MECHI Kuchezwa Mei 19 Allianz Arena, Munich

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad