Wanafunzi Watano wa Shule ya Msingi Kihinga,Ngara wafariki kwa Bomu wakiwa Shuleni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 08, 2017

Wanafunzi Watano wa Shule ya Msingi Kihinga,Ngara wafariki kwa Bomu wakiwa Shuleni.


Majeruhi wa Bomu hilo akitibiwa na Madaktari wa Hospitali ya Mission Rulenge,iliyopo wilayani Ngara.

Wanafunzi wa Tano  wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara  mkoani Kagera wamefariki dunia na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono  na wamelazwa Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo .

Mganga Mkuu wa hHospitali ya Rulenge, Sr Goleth Fredrick amesema idadi hiyo imeongezeka baada ya wengine kutolewa katika kituo cha afya bukiriro na kwamba wanafunzi wawili wamefariki wakati wakipatiwa Matibabu.




Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara  mkoani Kagera walionusurika wakiwa Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo.


Madaktari wa Hospitali ya Mission Rulenge wakiendelea na Matibabu kwa Majeruhi.

Kamanga wa Jeshi la Polosi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema chanzo cha wanafunzi hao kujeruhiwa kwa bomu ni zoezi la kuuza vyuma chakavu ambapo mwanafunzi aliliokota na kuja nalo shuleni ili alipeleke kwa mnunuzi na kupewa madaftari.

Hata hivyo Kamanda wa Kikosi cha Kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wilaya ya Ngara ,Meja TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa wangeleta athari zaidi .

Taarifa zaidi zinafuata


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad