Dk. Wilbrod Slaa ateuliwa na Rais Magufuli. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, November 24, 2017

Dk. Wilbrod Slaa ateuliwa na Rais Magufuli.

Dkt Wilbord Slaa alikuwa katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA –Tanzania.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Upinzani CHADEMA ameteuliwa kuwa Balozi na Rais wa Tanzania, Dkt.John Magufuli.

Katika taarifa ilitolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ,Gerson Msigwa, haijataja kituo chake cha kazi. Ila imeeleza "ataapishwa baada ya taratibu kukamilika"

Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka huo.

Slaa amekuwa katika siasa kwa zaidi ya miongo miwili na kabla ya hapo alikuwa padri wa kanisa katoliki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad