Kamati ya masaa 72:Yaipa Simba SC Pointi 3 za Kagera Sugar. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Friday, April 14, 2017

Kamati ya masaa 72:Yaipa Simba SC Pointi 3 za Kagera Sugar.

Toka Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya  akizungumza na Waandishi wa Habari Jana usiku April 13,2017 Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Bodi, Boniphace Wambura.

Klabu ya Simba SC imepewa Pointi 3 na magoli 3 baada ya kikao cha kamati ya Saa 72 -Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania kutokana na Rufaa waliyoikatia Kagera Sugar kwa kumtumia beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano katika mechi baina ya timu hizo Aprili 02, mwaka huu,2017.

Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba SC akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmed Yahya amewaambia Waandishi wa Habari usiku wa Jana April 13, 2017  Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kwamba Kamati ilibaini ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo la kikanuni na adhabu yake ni kupokonywa ushindi.

Kwa ushindi huo, Simba SC sasa inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 26, wakiendelea kuongoza kwenye Msimama wa Ligi Kuu Vodacom tanzania Bara 2016/2017 mbele ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 56 za mechi 25.

Ikumbukwe Simba SC iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kutokana na Kagera Sugar kumchezesha Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 iliyofanyika Aprili 02, 2017 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mohamed Fakhi picha hii ni wakati akiwa mchezaji wa Simba SC.

Kamati imejiridhisha kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alioneshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Majimaji, Mbeya City na African Lyon, hivyo hakustahili kucheza katika mchezo dhidi ya Simba uliyochezwa April 2 2017 uwanja wa Kaitaba na Simba ikapoteza kwa magoli 2-1.

Katika kikao chake awali Ijumaa iliyopita, Kamati baada ya kupitia malalamiko hayo, iliahirisha shauri hilo hadi leo kujipa muda wa kufuatilia baadhi ya vielelezo kuhusu malalamiko hayo.

Post Bottom Ad