Uwanja wa CCM Kirumba -Mwanza Sasa ruksa kutumika Mechi za Kimataifa. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 14, 2017

Uwanja wa CCM Kirumba -Mwanza Sasa ruksa kutumika Mechi za Kimataifa.

Shirikisho la soka duniani, FIFA na lile la Afrika, CAF kwa pamoja wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, kutumika kwenye mechi za kimataifa.

Kupitishwa kwa uwanja huo kumekuja baada ya wataalamu wa Ufundi wa CAF kwenda Mwanza kuukagua uwanja huo mwishoni mwa mwaka jana 2016.

Viwanja vingine ambavyo CAF na FIFA inavitambua nchini hadi sasa ni Amani wa Unguja, Zanzibar, Azam Complex na uwanja wa taifa wa Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake wa twitter  amebainisha  kuwa CAF na FIFA wameupitisha uwanja wa CCM Kirumba-mwanza utumike katika mechi za kimataifa, hivyo timu za Tanzania zitakuwa na uhuru wa kutumia uwanja wa Taifa au Kirumba.

Kupitishwa kwa CCM Kirumba kuna maana kuwa sasa mechi kubwa kama vile fainali za Kombe la Shirikisho, Ngao ya Hisani pamoja na mechi kubwa za kimataifa za kirafiki na mashindano ya CECAFA, CAF na FIFA ruksa kufanyika huko.

Viwanja vingine ambavyo vimekaguliwa na vinasubiri kupitishwa ni Gombani ulioko Pemba; Sokoine wa Mbeya na Kaitaba wa Kagera.

Post Bottom Ad