Mbwana Samatta aitandika 2-0 Botswana na kawapa Watanzania Furaha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 25, 2017

Mbwana Samatta aitandika 2-0 Botswana na kawapa Watanzania Furaha.

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Mbwana Samatta amefunga  magoli  2 wakati wakiwachakaza Timu ya Taifa ya Botswana  mabao 2-0 kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa leo March 25, 2017 kwenye  mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kalenda ya FIFA iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambayo miongoni mwa Wahudhuriaji wake ni Waziri mpya wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dokta Harison Mwakyembe.

Hii ilikuwa ni Mechi ya Kwanza kwa Kocha Mpya wa Taifa Stars, Salum Mayanga na Nahodha  Samatta kuipa bao Taifa Stars la kwanza dakika ya 3 tu ya mchezo huo  huku bao la pili likifungwa dakika ya 87 kwa Frikiki murua ya Samatta.
Licha ya kufunga magoli mawili, Samatta aliwa kwenye wakati mgumu kwa sababu mara nyingi alikuwa akichezewa rafu zilizosababisha wachezaji wa Botswana kuoneshwa kadi za njano. Samatta ilibidi atibiwe na daktari wa Stars baada ya kufanyiwa rafu wakati akijaribu kumtoka moja ya mabeki wa Botswana.

Botswana, chini ya Kocha Peter Buffler, ilionyesha Soka la kuridhisha lakini ukali wa Mchezaji wa Kulipwa Samatta, anaechezea Timu ya KRC Genk huko Belgium, ndio uliwaua.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Burundi Jumanne ijayo, Machi 28,2017.

Post Bottom Ad