Taswira ya mkutano wa CHADEMA wilaya ya Ngara kwa Kamanda Mawazo na Dr. Kabangira wakimpokea rasmi Dr.Bujari Uwanja wa Posta ya Zamani Mjini Ngara.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET

Post Top Ad

Sunday, December 29, 2013

Taswira ya mkutano wa CHADEMA wilaya ya Ngara kwa Kamanda Mawazo na Dr. Kabangira wakimpokea rasmi Dr.Bujari Uwanja wa Posta ya Zamani Mjini Ngara..

Mbunge wa Biharamulo Magharibi Dr.Anthony G.Mbassa akiwa ameshika furushi lililokusanywa kadi  za wanachama waliohamia CHADEMA kutoka vyama mbalimbali vya Siasa wilayani Ngara,katika mkutano wa Chadema uliofanyika viwanja vya posta ya zamani Mjini Ngara(Desemba 28,2013).

Anaepiga picha kwa simu ni Alphonce Mawazo (Kamanda Mawazo) alipojitoa CCM mwaka jana na madaraka makubwa tu CCM tena ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Sombetini Arusha na kujiunga Chadema ameamua kujikita Kanda ya ziwa kutoa elimu ya uraia na kueneza sera za Chadema na alikuwepo leo(Desemba 28,2013) katika jimbo la Ngara akiendeleza harakati za Chadema ni Msingi.

Baadhi ya Wenyeviti wa vitongo waliohamia CHADEMA (Desemba 28,2013) ni pamoja na ISSA MAGAMBO kitongoji cha Mulugunga,NESTORY SESHAHU lunyonga,MAYABAGABO kitongoji cha Kumutukula,katibu wa wilaya CUF,mgombea CCM-Ubunge kura ya maoni Dr.PETTER BUJARI kapokelewa rasmi leo,JENIROZA BARUNGULA wanawake wilaya NCCR-Mageuzi, Muhoza Mbunda Katibu kata CCM(mjini) na wengineo zaidi ya 20.

Pamoja na mambo mengine,Wananchi walitakiwa kutoogopa kudai haki yao kwa kuungana na CHADEMA kuchagua viongozi makini watakaoshirikiana nao kuleta mabadiliko ya kweli katika mahitaji yao ya msingi kama vile Elimu,Afya,Maji n.k pamoja na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata katiba mpya yenye manufaa kwa  watanzania na kuachana na propaganda zinazopandikizwa dhidi ya CHADEMA.

Ukiacha kadi nyingi zilizorejeshwa lakini mkutano huo huwezi kuuita mkutano wa hadhara bali ni sherehe ya mavuno ya kufungia mwaka 2013 kwa Chadema wilaya ya Ngara kupata wanachama wengi waliojiunga.

Pamoja na mambo mengine,Wananchi walitakiwa kutoogopa kudai haki yao kwa kuungana na CHADEMA kuchagua viongozi makini watakaoshirikiana nao kuleta mabadiliko ya kweli katika mahitaji yao ya msingi kama vile Elimu,Afya,Maji n.k pamoja na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata katiba mpya yenye manufaa kwa  watanzania na kuachana na propaganda zinazopandikizwa dhidi ya CHADEMA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad