Ligi Kuu Vodacom 2016/2017-Mechi za Mzunguko wa Pili - Yanga SC kileleni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 17, 2016

Ligi Kuu Vodacom 2016/2017-Mechi za Mzunguko wa Pili - Yanga SC kileleni.


Yanga SC imeshaifunga JKT Ruvu jumla ya magoli 29 katika mechi nane zilizopita huku yenyewe ikiruhusu magoli manne tu tangu mwaka 2013.

Yanga SC imepaa hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara 2016/2017 mara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya JKT Ruvu  katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili wa Ligi hiyo uliyoanza leo December 17,2016.

Ushindi dhidi ya JKT Ruvu unaifanya Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi  ifikishe jumla ya pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 pointi moja mbele ya mahasimu wao Simba  SC walio na pointi 35 ambao watacheza kesho Jumapili December 18,2016 dhidi ya Ndanda FC mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili ya VPL.

Deusi Kaseke alifunga goli la kwanza la Yanga SC dakika ya 37 kipindi cha kwanza kwa kuunganisha pasi ya Simon Msuva.

Msuva akafunga bao la pili dakika ya 57 kabla ya kufunga tena dakika ya 90 na kuilaza JKT Ruvu huku Yanga SC ikikaa kileleni mwa ligi ikisubiri matokeo ya Simba SC.

Ligi Kuu Vodacom -Mechi za Mzunguko wa Pili -Ratiba.

Jumamosi Desemba 17,2016.

JKT Ruvu 0 – 3 Yanga [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Mbeya City 0 – 0 Kagera Sugar [Sokoine, Mbeya]

Ruvu Shhoting 1 – 1  Mtibwa Sugar [Mabatini, Mlandizi]

Mwadui FC 1 – 0 Toto African [Mwadui Complex, Mwadui]


Jumapili Desemba 18,2016.

Mbao FC v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]

Ndanda FC v Simba [Nangwanda, Mtwara]

African Lyon v Azam FC [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Tanzania Prisons v Majimaji FC [Sokoine, Mbeya]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad