LEWIS GABRIEL Toka Kata ya Chanika wilayani Karagwe/Kagera Ndiye Mshindi wa RADIO KARAGWE STAR SEARCH 2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 17, 2016

LEWIS GABRIEL Toka Kata ya Chanika wilayani Karagwe/Kagera Ndiye Mshindi wa RADIO KARAGWE STAR SEARCH 2016.


Pichani ni Mashabiki wa Msanii LEWIS GABRIEL Kutoka Kata ya Chanika wilayani Karagwe wakifurahia ushindi wa Msanii wao huyo aliyeibuka kidume katika Shindano la Kituo cha Radio Karagwe kilichopo wilayani Karagwe mkoani Kagera kupitia Shindano la RADIO KARAGWE STAR SEARCH 2016 ambapo aliwashinda washiriki wenzake kwa kupata asilimia 96 YA Kura za Majaji.

Fainali ya mashindano hayo imefanyika jana Ijumaa December 16,2016 na Vigezo vilivytazamwa na Majaji kwa Washiriki wote 31 kutoka wilaya nne za mkoa wa Kagera za Karagwe, Misenyi, kyerwa na Bukoba vijijini  ni pamoja na Muonekano, Ubunifu, maudhui ya wimbo/ujumbe, melod/ghani, hamasa, Uchangamfu na kutawala jukwaa, Uwezo wa kutoa sauti halisi.
Aidha kuelekea Fainali hiyo,Jumla ya washiriki nane waliingia katika  hatua hiyo na Matokeo kutolewa kama ifatavyo.

MSHINDI WA KWANZA: Lewis Gabriel 96% -Kata ya Chanika wilaya ya Karagwe. 

MSHINDI WA PILI: Efatha Band 76% -Kutoka  wilaya Kyerwa. 


MSHINDI WA TATU:Merchades Kazoba 70% -Kutoka wilaya ya Kyerwa.

Mgeni rasmi Mhe. Karim Amri ambaye ni MNEC Wilaya ya Karagwe (Pichani kushoto ) Katika fainali hiyo ya  RADIO KARAGWE STAR SEARCH 2016  pamoja na kutoa Zawadi ya cheti kwa washiriki wote.

Licha ya kuwapongeza Washiriki wote kwa kushiriki vyema na kuoneshana ushindani kupitia vipaji vyao aliwataka Washiriki wa shindano hilo kutunga wimbo kuhusu Utunzaji  wa mazingira na uhifadhi wake, na kuahidi kuudhamini wimbo huo na video yake ili kuhamasisha Wana Karagwe kuhifadhi na kutunza mazingira
Mgeni rasmi Mhe. Karim Amri ambaye ni MNEC Wilaya ya Karagwe (Pichani kulia)sambamba na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe na Diwani wa kata ya Rugera Mhe.Dawson Byamanyilohi wakifatilia kwa umakini shindano hilo.


Meza ya Majaji wakati wa shindano la Radio Karagwe Star Search 2016 lililohitimishwa jana December 16,2016 Mjini Kayanga,Karagwe.

Washiriki kama kawaida walipandishwa Kikaangoni kujajiwa.


Mashabiki hawakuwa nyuma nao kufatilia kila kitu wakati wa fainali hiyo.





Pichani juu na chini ni Mgeni rasmi Mhe. Karim Amri ( (Pichani kulia) ambaye ni MNEC Wilaya ya Karagwe akigawa zawadi ya Vyeti kwa Washiriki nane wa fainali katika shindano hilo.





Kutoka katikati ni Mkurugenzi wa Radio Karagwe, Dkt. Godfrey Aligawesa,pamoja na kuwashukuru wadau kwa kuchangia udhamini wao na kuhudhuria,amesema  lengo lilikuwa ni kumpata msanii chipukizi atakayesimamiwa na Kituo hicho cha redio  kurekodi  wimbo wake atakaokuwa ameutunga na album yake.

kushoto ni Bw. Shaban Ngallama Afisa uzalishaji Vipindi Radio Karagwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad