Waandishi wa Habari kutoka Redio 5 za Kijamii Wajengewa uwezo kupitia Kampeni ya’’ ZUIA AJALI HAPA ‘’ ili kupunguza ajali Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, December 15, 2016

Waandishi wa Habari kutoka Redio 5 za Kijamii Wajengewa uwezo kupitia Kampeni ya’’ ZUIA AJALI HAPA ‘’ ili kupunguza ajali Mkoani Kagera.

Bw.Joseph Sekiku,Mkurugenzi wa Radio FADECO ya wilayani Karagwe,mkoani Kagera akitoa Somo la ALAMA Muhimu za Barabarani kwa Washiriki 9 wa mafunzo   kutoka Redio 5 za Kijamii mkoani Kagera ,(Radio FADECO,RADIO KWIZERA,RADIO KASIBANTE,RADIO KARAGWE NA RADIO VISSION) kupitia Kampeni ya ZUIA AJALI HAPA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Lengo ni  kuhamasisha Wananchi Mkoani Kagera kuripoti na kukemea Vitendo vya uvunjifu wa sharia za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Mkufunzi mkuu,Mwalimu Josephat Mwanzi -kushoto akifatilia uchangiaji wa mada Juu ya  Kampeni ya ZUIA AJALI HAPA Moani Kagera kutoka kwa Washiriki wa Radio 5 za Kijamii Mkoani Kagera .

Washiriki wa Mafunzo kutoka Redio 5 za Kijamii mkoani Kagera ,(Radio FADECO,RADIO KWIZERA,RADIO KASIBANTE,RADIO KARAGWE NA RADIO VISSION) wakijengewa Uwezo Kuandaa Vipindi na Kuripoti Habari za kupitia  Kampeni ya ZUIA AJALI HAPA ili kupunguza ajali Nchini.



UTANGULIZI.  

Kufuatia ongezeko wa matukio ya ajali za barabarani mkoani Kagera, Radio FADECO imeamua kushiriki, kuwashirikisha na kuunga mkono jitihada zinazofanywa kutokomeza ajali za barabarani kwa kuwaalika wadau wote wa usalama barabarani mkoani Kagera na pengineko, kuungana katika kampeini ya ZUIA AJALI HAPA kwa kutoa elimu ya usalama barabarani kupitia SHULE ZOTE ZA MSINGI, SEKONDARI na VYUO VYA ELIMU YA JUU NA UFUNDI mkoani Kagera. 

Pamoja na kuendesha na kuruhusu vipindi vya usalama barabani redioni mara moja kwa wiki, sasa RADIO FADECO kwa Kushirikiana na Radio nyingine za Mkoani Kagera kuendeleza kampeini hii mashuleni. 
  
KWA NINI KUELEKEZA MKAKATI WA ELIMU YA USALAMA BARABARANI MASHULENI (SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI, VYUO VYA ELIMU YA UFUNDI NA YA JUU)? 

Wanafunzi kama WAHANGA WAKUU NA WALENGWA MAHUSUSI: 

Wanafunzi kama sehemu ya watumia barabara na walengwa wakuu wa usalama barabarani, hawana budi kuelimishwa juu ya usalama barabarani,  

·        kwani kila siku wanatumia barabara wanapokwenda shule au wanaporudi kutoka shuleni. 

·        Kwa kuwa wanatumia barabara kila siku, hawana budi kuzifahamu na kuzifuata sheria za usalama barabarani. 

·         Wao pia kama abiria wakiwa wakisafiri, wanakuwa na jukumu la kusaidia katika kuelimisha, kukumbushia na kufuatilia matumizi ya sheria na kanuni za usalama barabarani. 

·         Lakini wao pia kama madreva wa kesho, ni vema waanze harakati za kupata leseni za udreva wakiwa tayari wanazijua sheria na kanuni za usalama barabarani (si kama inavyokuwa siku hizi katika vyuo vya udereva, kuanza kufundisha alama za usalama barabarani, n.k.) 

KAMA WAKUFUNZI WA WENZAO NA JAMII KWA UJUMLA HUSUSANI WAZAZI WAO (PEER EDUCATORS) 

Wanafunzi wanakuwa WAKUFUNZI wazuri kwa wazazi na ndugu zao wa karibu, na kwa wananchi wote kwa ujumla, hivyo tukipandikiza mbegu ya kutii sharia za usalama barabarani kwao, tunakuwa tumepandika mbegu ya kudumu. 

SHULE ZINATOA FURSA YA MIKUSANYIKO MIKUBWA KWA WAKATI MOJA KILA SIKU (SCHOOLS PROVIDE OPPORTUNITY FOR MASS GATHERING IDEAL FOR MASS SENSITIZATION CAMPAIGNS) 

Shule zote ziwe za msingi, sekondari au vyuo, zina mkusanyiko na idadi kubwa wa watu kwa kila wakati. 

Zipo shule zenye wanafunzi kuanzia 100 huku zingine zina wanafunzi zaidi ya 500.

 Mkusanyiko huu unaopatikana kwa wakati moja na kila siku, ni fursa kubwa ya kutoa hamasa na elimu ya usalama barabarani.    

MPANGO WA RADIO FADECO NA WADAU (PROPOSED PLAN OF FADECO RADIO WITH PARTNERS): 

1. Kushirikiana na wadau wote wa usalama barabarani na wa maendeleo na wananchi wote kwa ujumla katika kampeini hii ya ZUIA AJALI HAPA. Wadau hawa ni pamoja na JESHI LA POLICE, VYUO VYA UDEREVA, WAHISANI NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA. 

2. Kutengeneza na kusambaza vibao na vipeperushi vya alama za usalama barabani kuanzia kila shule ya msingi, sekondari na vyuo. 

Na baadae katika kila ofisi ya serikali na sehemu yeyote yenye mkusanyiko mfano dispensary, hospitali, ofisi za serikali na taasisi. 

3. Kuomba Idara ya elimu ya mkoa na wilaya pamoja na uongozi wa shule, kuruhusu kuanzisha KIRANJA wa usalama barabarani katika kila shule. KIRANGA HUYU atakuwa kama AFISA USALAMA BARABARANI katika kila shule. 

Atafundishwa Zaidi kusimamia usalama wa wanafunzi wenzake katika shule husika. Atapewa vazi rasmi la usalama barabarani la kumutambulisha na ataombwa kulivaa kila siku anapokuwa shuleni au akitoka nyumbani kuja shule. 

4. Kuendesha vipindi vya usalama barabarani redioni kila wakati 5. Kuomba ushiriki wa RADIO ZOTE za mkoa wa kagera (RADIO KWIZERA, FADECO, KASIBANTE, KARAGWE na RADIO VISION) kushiriki katika kampeini hii. 

Kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari na watangazaji jinsi ya kutoa taarifa na elimu juu ya usalama barabarani. 

6. Kusaidiana na wadau wa usalama barabarani katika kuhakikisha kuwa, tunaanzisha mitandao ya ROAD SAFETY AMBASSADORS katika ngazi ya kila wilaya. 

7. Kuanzisha utaratibu wa kupashana taarifa za usalama barabarani kwa njia ya Radio au TEHAMA.  

Walengwa:  Shule za Msingi 925  Shile za sekondari 345  Vyuo vya elimu ya juu   37 

WADAU KATIKA KAMPENI HII.

RADIO ZA JAMII NA ZINGINE MKOANI KAGERA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI, JESHI LA POLISI KAGERA KAMATI ZA USALAMA BARABARANI ZA WILAYA ZOTE KAGERA VYUO VYA MAFUNZO YA UDEREZA IDARA YA ELIMU NA SHULE ZOTE MKOANI KAGERA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad